Zaburi 100:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC5 Maana BWANA ni mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake katika vizazi vyote. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema5 Mwenyezi-Mungu ni mwema; fadhili zake zadumu milele, na uaminifu wake katika vizazi vyote. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND5 Mwenyezi-Mungu ni mwema; fadhili zake zadumu milele, na uaminifu wake katika vizazi vyote. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza5 Mwenyezi-Mungu ni mwema; fadhili zake zadumu milele, na uaminifu wake katika vizazi vyote. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu5 Kwa maana Mwenyezi Mungu ni mwema na fadhili zake zadumu milele; uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu5 Kwa maana bwana ni mwema na upendo wake wadumu milele; uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote. Tazama sura |
hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru BWANA nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu BWANA, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya BWANA,
itasikika tena sauti ya furaha na sauti ya shangwe, sauti ya bwana arusi na sauti ya bibi arusi, sauti yao wasemao Mshukuruni BWANA wa majeshi, maana BWANA ni mwema, rehema zake ni za milele; na sauti zao waletao sadaka za shukrani nyumbani kwa BWANA. Kwa kuwa nitawarudisha wafungwa wa nchi hii kama kwanza, asema BWANA.