Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 100:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 Mtumikieni BWANA kwa furaha; Njoni mbele zake mkiimba;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Mwabuduni Mwenyezi-Mungu kwa furaha, nendeni kwake mkiimba kwa shangwe!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Mwabuduni Mwenyezi-Mungu kwa furaha, nendeni kwake mkiimba kwa shangwe!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Mwabuduni Mwenyezi-Mungu kwa furaha, nendeni kwake mkiimba kwa shangwe!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Mwabuduni Mwenyezi Mungu kwa furaha; njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Mwabuduni bwana kwa furaha; njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.

Tazama sura Nakili




Zaburi 100:2
15 Marejeleo ya Msalaba  

Hata siku ya nane akaagana na watu, nao wakambarikia mfalme, wakaenda hemani kwao, wakifurahi na kuchangamka moyoni kwa wema wote BWANA aliomfanyia Daudi mtumishi wake, na Israeli watu wake.


Tena Hezekia mfalme na wakuu wakawaamuru Walawi, wamwimbie BWANA sifa kwa maneno ya Daudi, na ya Asafu mwonaji. Wakaimba sifa kwa furaha, wakainamisha vichwa, wakaabudu.


Hezekia akaziweka zamu za makuhani na Walawi kwa zamu zao, kila mtu kwa kadiri ya huduma yake, makuhani na Walawi pia, kwa sadaka za kuteketezwa na kwa sadaka za amani, kutumika, na kushukuru, na kusifu, malangoni mwa kambi ya BWANA.


Nayakumbuka mambo haya kwa uchungu moyoni mwangu, Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano, Na kuwaongoza hadi katika nyumba ya Mungu, Kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu.


Midomo yangu itafurahi sana nikuimbiapo, Na nafsi yangu uliyoikomboa.


Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi.


Nanyi mtafurahi mbele za BWANA, Mungu wenu, ninyi, na wana wenu, na binti zenu, na watumishi wenu wa kiume na wa kike, na Mlawi aliyemo malangoni mwenu; kwa kuwa hana sehemu wala urithi kwenu.


nawe utafurahi mbele ya BWANA, Mungu wako, wewe na mwana wako na binti yako, na mtumwa wako na mjakazi wako, na Mlawi aliye ndani ya malango yako, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio katikati yako, katika mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake.


nawe utafurahi katika sikukuu yako, wewe, na mwanao, na binti yako, na mtumwa wako, na mjakazi wako, na Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako.


kwa kuwa hukumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa furaha na moyo wa kushukuru, kwa ajili ya ule wingi wa vitu vyote;


Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo