Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 10:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

16 BWANA ndiye Mfalme milele na milele; Mataifa yataangamia kutoka nchi yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Mwenyezi-Mungu ni mfalme milele na milele! Mataifa yasiyomjua yatatoweka nchini mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Mwenyezi-Mungu ni mfalme milele na milele! Mataifa yasiyomjua yatatoweka nchini mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Mwenyezi-Mungu ni mfalme milele na milele! Mataifa yasiyomjua yatatoweka nchini mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Mwenyezi Mungu ni Mfalme milele na milele, mataifa wataangamia watoke nchini mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 bwana ni Mfalme milele na milele, mataifa wataangamia watoke nchini mwake.

Tazama sura Nakili




Zaburi 10:16
20 Marejeleo ya Msalaba  

Ee BWANA, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na ushindi, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee BWANA, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote.


Ufalme wako ni ufalme wa milele, BWANA ni mwaminifu katika maneno yake yote, Na mwenye fadhili katika matendo yake yote Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.


BWANA atamiliki milele, Mungu wako, Ee Sayuni, kwa vizazi vyote. Haleluya.


BWANA aketi juu ya Gharika; Naam, BWANA ameshika hatamu ya ufalme milele.


Akawafukuza mataifa mbele yao, Akawapimia urithi kwa kamba, Na kuwakalisha makabila ya Israeli katika hema zao.


Mataifa wamezama katika shimo walilolichimba; Kwa wavu waliouficha imenaswa miguu yao.


Umewakemea mataifa; Na kumwangamiza mdhalimu; Umelifuta jina lao milele na milele;


Naye atauhukumu ulimwengu kwa haki; Atawaamua watu kwa uadilifu.


BWANA ametamalaki, amejivika adhama, BWANA amejivika, ukuu na nguvu, kama mavazi ya kifalme. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;


BWANA atatawala milele na milele.


Kwa maana BWANA ndiye mwamuzi wetu; BWANA ndiye mfanya sheria wetu; BWANA ndiye mfalme wetu; ndiye atakayetuokoa.


Bali BWANA ndiye Mungu wa kweli; Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele; Mbele za ghadhabu yake nchi yatetemeka, Wala mataifa hawawezi kustahimili hasira yake.


Wewe, BWANA, unadumu milele; Kiti chako cha enzi ni tangu kizazi hata kizazi.


Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadneza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi;


Mimi ninaweka amri, ya kwamba katika mamlaka yote ya ufalme wangu watu watetemeke na kuogopa mbele za Mungu wa Danieli; maana yeye ndiye Mungu aliye hai, adumuye milele, na ufalme wake ni ufalme usioharibika, na mamlaka yake itadumu hata mwisho.


Kama vile mataifa yale ambayo BWANA anawaangamiza mbele yenu, ndivyo mtakavyoangamia; kwa sababu hamkutaka kuisikiliza sauti ya BWANA, Mungu wenu.


Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo