Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Yoshua 16:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

3 kisha ikateremkia upande wa magharibi hadi kuufikia mpaka wa Wayafleti, hadi mpaka wa Beth-horoni ya chini, hadi kufikia Gezeri; na matokeo yake yalikuwa hapo baharini.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Kisha ukashuka magharibi katika nchi ya Wayafleti hadi Beth-horoni ya Chini na Gezeri na kuishia kwenye bahari ya Mediteranea.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Kisha ukashuka magharibi katika nchi ya Wayafleti hadi Beth-horoni ya Chini na Gezeri na kuishia kwenye bahari ya Mediteranea.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Kisha ukashuka magharibi katika nchi ya Wayafleti hadi Beth-horoni ya Chini na Gezeri na kuishia kwenye bahari ya Mediteranea.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 ukateremkia kuelekea magharibi hadi eneo la Wayafleti ukienea hadi eneo la Beth-Horoni ya Chini hadi Gezeri, ukiishia baharini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 ukateremkia kuelekea magharibi hadi eneo la Wayafleti ukienea hadi eneo la Beth-Horoni ya Chini hadi Gezeri, ukiishia baharini.

Tazama sura Nakili

Yoshua 16:3
9 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa baada ya hayo, kulitokea vita na Wafilisti huko Gezeri; ndipo Sibekai, Mhushathi, alipomwua Safu, mmojawapo wa Warefai; nao Wafilisti wakashindwa.

Na binti yake alikuwa Sheera, ambaye alijenga Beth-horoni, wa chini na wa juu, na Uzen-sheera.

Na hizi ndizo miliki yao na makao yao; Betheli na vijiji vyake, na upande wa mashariki Naara, na upande wa magharibi Gezeri na vijiji vyake; na Shekemu pia na vijiji vyake, hata Aza na vijiji vyake;

Tena akaujenga Beth-horoni wa juu, na Beth-horoni wa chini, miji yenye boma, yenye kuta, na malango, na makomeo;

Kisha mpaka wenu wa upande wa magharibi mtakuwa na bahari kubwa na mpaka wake; huu ndio mpaka wenu upande wa magharibi.

Wakati huo Horamu, mfalme wa Gezeri, akakwea ili kuusaidia Lakishi, lakini Yoshua akampiga yeye na watu wake, hata asimsazie hata mtu mmoja.

Kisha mpaka ukaendelea kutoka hapo na kufikia mji wa Luzu, ubavuni mwa Luzu (ndio Betheli), kwa upande wa kusini; kisha mpaka ukateremkia Ataroth-adari, karibu na mlima ulio upande wa kusini wa Beth-horoni wa chini.

na kikosi kingine kikageukia njia iendayo Beth-horoni; na kikosi kingine kikageukia njia ya mpakani ielekeayo bonde la Seboimu upande wa nyika.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo