Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 8:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Mizizi yake huzongazonga chuguu, Huangalia mahali penye mawe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Mizizi yake hujisokotasokota kwenye mawe naye aenda kuchunguza ndani ya mwamba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Mizizi yake hujisokotasokota kwenye mawe naye aenda kuchunguza ndani ya mwamba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Mizizi yake hujisokotasokota kwenye mawe naye aenda kuchunguza ndani ya mwamba.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 huifunganisha mizizi yake kwenye lundo la mawe, na kutafuta nafasi kati ya mawe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 huifunganisha mizizi yake kwenye lundo la mawe, na kutafuta nafasi katikati ya mawe.

Tazama sura Nakili




Yobu 8:17
9 Marejeleo ya Msalaba  

Chini, mizizi yake itakaushwa; Na juu, tawi lake litasinyaa.


Shina langu limeenea hata kufika majini, Na umande hukaa usiku kucha katika matawi yangu;


Yeye huwa mti mbichi mbele ya jua, Nayo machipukizi yake huenea katika bustani yake.


Lakini, aking'olewa mahali pake, Ndipo patamkana, na kusema, Mimi sikukuona.


Naam, hawakupandwa; hawakutiwa katika ardhi kama mbegu; naam, shina lao halikutia mizizi katika ardhi; tena awapuzia tu, wakanyauka, upepo wa kisulisuli wawaondoa kama mabua makavu.


Kwa hiyo kama vile muali wa moto uteketezavyo mabua makavu, na kama manyasi makavu yaangukavyo katika muali wa moto; kadhalika shina lao litakuwa kama ubovu, na ua lao litapeperushwa juu kama mavumbi; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA wa majeshi, na kulidharau neno lake aliye Mtakatifu wa Israeli.


Na asubuhi walipokuwa wakipita, waliuona ule mtini umenyauka toka shinani.


Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung'olewa kabisa;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo