Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 8:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Ndivyo ulivyo mwisho wa hao wamsahauo Mungu; Na matumaini yake huyo mbaya huangamia;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Ndivyo walivyo wote wanaomsahau Mungu. Tumaini la wasiomwamini Mungu litapotea.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Ndivyo walivyo wote wanaomsahau Mungu. Tumaini la wasiomwamini Mungu litapotea.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Ndivyo walivyo wote wanaomsahau Mungu. Tumaini la wasiomwamini Mungu litapotea.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Huu ndio mwisho wa watu wote wanaomsahau Mungu; vivyo hivyo matumaini ya wasiomjali Mungu huangamia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Huu ndio mwisho wa watu wote wanaomsahau Mungu; vivyo hivyo matumaini ya wasiomjali Mungu huangamia.

Tazama sura Nakili




Yobu 8:13
25 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini macho ya waovu yataingia kiwi, Nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia, Na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho.


Hili nalo litakuwa ni wokovu wangu; Kwani asiyemcha Mungu hatakaribia mbele yake.


Kwa kuwa jamii ya hao wasiomcha Mungu watakuwa tasa, Na moto utateketeza mahema yenye rushwa.


Atang'olewa katika hema yake aliyokuwa akiitumaini; Naye atapelekwa kwake mfalme wa vitisho.


Ya kuwa shangwe ya waovu ni kwa muda kidogo, Na furaha ya wapotovu ni ya dakika moja tu?


Lakini hao wasiomcha Mungu mioyoni hujiwekea hasira Hawalilii msaada hapo awafungapo.


Yakiwa yangali mabichi bado, wala hayakukatwa, Hunyauka mbele ya majani mengine.


Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.


Mdhalimu kwa kiburi cha uso wake Asema, Mungu Hatapatiliza. Mawazo yake yote ni, Hakuna Mungu;


Asiye haki ataona na kusikitika, Atasaga meno yake na kuondoka, Matumaini ya wasio haki hupotea.


Yafahamuni hayo, Ninyi mnaomsahau Mungu, Nisije nikawararueni, Asipatikane wa kuwaokoa.


Wadhalimu wataenda kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.


Matumaini yao wenye haki yatakuwa furaha; Bali matarajio yao wasio haki yatapotea.


Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake linapotea; Na matumaini ya uovu huangamia.


Waovu huangamia, hata hawako tena; Bali nyumba ya mwenye haki itasimama.


Wenye dhambi walio katika Sayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wasiomcha Mungu; Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uangamizao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele?


Ukamsahau BWANA, Muumba wako, yeye aliyezitanda mbingu, na kuiweka misingi ya dunia; nawe unaogopa daima mchana kutwa kwa sababu ya ghadhabu yake yeye aoneaye, hapo ajitayarishapo kuharibu; nayo i wapi ghadhabu yake aoneaye?


Nikasema, Nguvu zangu zimepotea, Na tumaini langu kwa BWANA.


atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.


ndipo ujitunze, usije ukamsahau BWANA aliyekutoa nchi ya Misri, nyumba ya utumwa.


Jihadhari, usije ukamsahau BWANA, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake, ninazokuamuru leo.


basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau BWANA, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa;


Lakini itakuwa, kama ukimsahau BWANA, Mungu wako, na kuiandama miungu mingine, na kuitumikia na kuiabudu, nawaonya leo ya kuwa mtaangamia bila shaka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo