Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yobu 6:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Nguvu zangu ni zipi, hata ningoje? Na mwisho wangu ni nini, hata nisubiri?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Lakini sina nguvu ya kuweza kuendelea; sijui mwisho wangu utakuwaje, nipate kuvumilia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Lakini sina nguvu ya kuweza kuendelea; sijui mwisho wangu utakuwaje, nipate kuvumilia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Lakini sina nguvu ya kuweza kuendelea; sijui mwisho wangu utakuwaje, nipate kuvumilia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 “Nina nguvu gani, hata niendelee kutumaini? Matazamio yangu ni nini, hata niendelee kuwa mvumilivu?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 “Ninazo nguvu gani, hata niendelee kutumaini? Matazamio yangu ya mbele ni nini, hata niendelee kuwa mvumilivu?

Tazama sura Nakili




Yobu 6:11
15 Marejeleo ya Msalaba  

Je! Siku zangu si chache? Acha basi, Usinisumbue, nipate angaa kutulizwa moyo kidogo.


Je! Utalitaabisha jani lipeperushwalo? Au, je! Utayafuatia hayo mabua makavu?


Nijapokuwa ni kama kitu kilichooza, kinachosinyaa, Mfano wa nguo iliyoliwa na nondo.


Roho yangu imezimia, siku zangu zimekoma, Kaburi i tayari kunipokea.


Nikitazamia kuzimu kuwa nyumba yangu; Nikitandika malazi yangu gizani;


Mimi, je! Mashitaka yangu yamhusu mwanadamu? Nami kwa nini nisikose kusubiri?


Jinsi ulivyomsaidia huyo asiye na uwezo! Jinsi ulivyouokoa mkono usio na nguvu!


Je! Nguvu zangu ni nguvu za mawe? Au mwili wangu, je! Ni shaba?


Amezipunguza nguvu zangu njiani; Amezifupisha siku zangu.


BWANA, unijulishe mwisho wangu, Na idadi ya siku zangu ni ngapi; Nijue jinsi maisha yangu yalivyo mafupi.


Tazama, umefanya siku zangu kuwa mashubiri; Maisha yangu ni kama si kitu mbele zako. Kila mwanadamu, ingawa amesitawi, ni ubatili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo