Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 39:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 Ni nani aliyemwacha pundamilia aende huru? Au je! Ni nani aliyemfungulia vifungo punda mwitu?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 “Nani aliyemwacha huru pundamwitu? Nani aliyewaacha waende kwa kuwafungua?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 “Nani aliyemwacha huru pundamwitu? Nani aliyewaacha waende kwa kuwafungua?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 “Nani aliyemwacha huru pundamwitu? Nani aliyewaacha waende kwa kuwafungua?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 “Ni nani aliyemwachia punda-mwitu awe huru? Ni nani aliyezifungua kamba zake?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 “Ni nani aliyemwachia punda-mwitu awe huru? Ni nani aliyezifungua kamba zake?

Tazama sura Nakili




Yobu 39:5
13 Marejeleo ya Msalaba  

Naye atakuwa kama punda mwitu kati ya watu, mkono wake utapingana na watu wote na mkono wa kila mtu ukipingana naye; na ataishi kwa ugomvi na jamaa yake yote.


Isakari ni punda hodari, Ajilazaye kati ya mazizi ya kondoo;


Lakini mpumbavu aweza kupata ufahamu, Ingawa mwanadamu huzaliwa kama mtoto wa punda mwitu.


Tazama, kama punda mwitu jangwani Wao hutoka kwenda kazini mwao, wakitafuta chakula kwa bidii; Jangwa huwapa chakula cha watoto wao.


Je! Waweza kumfunga nyati kwa kamba matutani? Au, yeye atayalima mabonde nyuma yako?


Watoto wao wako katika hali nzuri, hukua katika bara wazi; Huenda zao, wala hawarudi tena.


Je! Huyo punda mwitu hulia akiwa na majani? Au, ng'ombe hulia akiwa malishoni?


Zamnywesha kila mnyama wa porini; Kwayo punda mwitu huzima kiu yao.


maana jumba la mfalme litaachwa; mji uliokuwa na watu wengi utakuwa hauna mtu; kilima na mnara utakuwa makao ya wanyama milele, furaha ya punda mwitu, malisho ya makundi ya kondoo;


Na punda mwitu husimama juu ya vilele vya milima, Hutwetea pumzi kama mbwamwitu; Macho yao hayaoni sawasawa, Kwa kuwa hapana majani.


punda wa mwitu aliyeizoelea nyika, avutaye pumzi za upepo katika tamaa yake; katika wakati wake ni nani awezaye kumgeuza? Wote wamtafutao hawatajichosha nafsi zao; katika mwezi wake watamwona.


Akafukuzwa mbali na wanadamu, moyo wake ukafanywa kuwa kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa pamoja na punda mwitu; akalishwa majani kama ng'ombe, mwili wake ukalowa maji kwa umande wa mbinguni; hata alipojua ya kuwa Mungu Aliye Juu ndiye anayetawala katika ufalme wa wanadamu, na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye yote.


Kwa maana wamekwea kwenda Ashuru, mfano wa punda wa porini aliye peke yake; Efraimu ameajiri wapenzi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo