Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 39:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Bawa la mbuni hufurahi; Lakini mabawa yake na manyoya yake, je! Yana huruma?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 “Mbuni hupigapiga mabawa yake kwa madaha, lakini hawezi kuruka kama korongo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 “Mbuni hupigapiga mabawa yake kwa madaha, lakini hawezi kuruka kama korongo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 “Mbuni hupigapiga mabawa yake kwa madaha, lakini hawezi kuruka kama korongo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 “Mbuni hupigapiga mabawa yake kwa furaha, lakini hayawezi kulinganishwa na mabawa na manyoya ya korongo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 “Mbuni hupigapiga mabawa yake kwa furaha, lakini hayawezi kulinganishwa na mabawa na manyoya ya korongo.

Tazama sura Nakili




Yobu 39:13
10 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa mfalme alikuwa na merikebu za Tarshishi baharini pamoja na merikebu za Hiramu; mara moja katika miaka mitatu huja merikebu za Tarshishi, zikileta dhahabu, na fedha, na pembe, na nyani, na tausi.


Kwa kuwa mfalme alikuwa na merikebu zilizokwenda Tarshishi pamoja na watumishi wa Hiramu; mara moja katika miaka mitatu huja merikebu za Tarshishi, zikileta dhahabu, na fedha, na pembe, na nyani, na tausi.


Mimi ni ndugu yao mbwamwitu, Ni mwenzao mbuni.


Je! Utamtumaini kwamba ataileta mbegu yako nyumbani. Na kukusanya nafaka ya kiwanja chako cha kupuria?


Kwa maana yeye huyaacha mayai yake juu ya nchi, Na kuyatia moto mchangani,


Humo ndege hujenga viota vyao, Korongo, anayo makao katika misonobari.


Naam, koikoi angani ajua nyakati zake zilizoamriwa; na hua na mbayuwayu na korongo huangalia wakati wa kuja kwao; bali watu wangu hawazijui amri za BWANA.


na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake;


na korongo, na koikoi kwa aina zake, na hudihudi, na popo.


Ndipo nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, wanawake wawili walitokea, nao upepo ulikuwa katika mabawa yao; na mabawa yao yalikuwa kama mabawa ya korongo; wakaiinua ile efa kati ya dunia na mbingu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo