Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 38:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Hapo Mwenyezi-Mungu alimjibu Yobu kutoka dhoruba:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Hapo Mwenyezi-Mungu alimjibu Yobu kutoka dhoruba:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Hapo Mwenyezi-Mungu alimjibu Yobu kutoka dhoruba:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Kisha Mwenyezi Mungu akamjibu Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli. Akasema:

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Kisha bwana akamjibu Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli. Akasema:

Tazama sura Nakili




Yobu 38:1
16 Marejeleo ya Msalaba  

tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, ndege, na mnyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi; wote wanaotoka katika safina, hata kila kilicho hai katika nchi.


Akasema, Toka, usimame mlimani mbele za BWANA. Na tazama, BWANA akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunjavunja miamba mbele za BWANA; lakini BWANA hakuwamo katika upepo ule; na baada ya upepo, tetemeko la nchi; lakini BWANA hakuwamo katika lile tetemeko la nchi;


Ikawa, hapo BWANA alipokuwa karibu kumchukua Eliya mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Eliya alitoka Gilgali pamoja na Elisha.


Ikawa, walipokuwa wakiendelea mbele na kuongea, tazama! Kukatokea gari la moto, na farasi wa moto, likawatenga wale wawili; naye Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli.


Lakini, laiti Mungu angenena, Na kuifunua midomo yake juu yako;


Amepiga duara kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji, Hata hapo mwanga na giza vinapopakana.


Sikiliza neno hili, Ee Ayubu; Simama kimya, uzifikiri kazi za Mungu za ajabu.


Dhoruba hutoka katika vyumba vyake; Na baridi ghalani mwake.


BWANA akafululiza kumjibu Ayubu, na kusema,


Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,


Nikaona, na tazama, upepo wa dhoruba ulitoka upande wa kaskazini, wingu kubwa sana, pamoja na moto, ukifanya duara ya nuru, na mwangaza pande zote, na katikati yake kitu kama rangi ya kaharabu, katikati ya moto huo.


BWANA si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; BWANA ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo