Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 37:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

22 Kaskazini hutokea mng'ao wa dhahabu; Mungu huvikwa ukuu utishao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Mngao mzuri hutokea kaskazini; Mungu amezungukwa na utukufu wa kutisha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Mngao mzuri hutokea kaskazini; Mungu amezungukwa na utukufu wa kutisha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Mng'ao mzuri hutokea kaskazini; Mungu amezungukwa na utukufu wa kutisha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Kutoka kaskazini yeye huja na fahari kuu; Mungu huja katika utukufu wa kutisha.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Kutoka kaskazini yeye huja na fahari kuu; Mungu huja katika utukufu wa kutisha.

Tazama sura Nakili




Yobu 37:22
22 Marejeleo ya Msalaba  

Ee BWANA, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na ushindi, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee BWANA, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote.


Na sasa watu hawawezi kuutazama mwanga ung'aao mbinguni; Lakini upepo ukipita huzitakasa.


Yeye Mwenyezi hamwezi kumwona; Yeye ni mkuu mwenye uweza; Tena mwenye hukumu, na mwingi wa haki, hataonea.


Haya! Jivike sasa fahari na ukuu; Jipambe heshima na enzi.


Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Wewe, BWANA, Mungu wangu, Umejifanya mkuu sana; Umejivika heshima na utukufu.


Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako, Na matendo yako yote ya ajabu.


Sauti ya BWANA ina nguvu; Sauti ya BWANA ina utukufu;


Njoni myaone matendo ya Mungu; Hutisha kwa mambo awatendayo wanadamu;


Mungu ni mwenye kutisha Kutoka patakatifu pako. Ndiye Mungu wa Israeli; Yeye huwapa watu wake nguvu na uwezo. Na ahimidiwe Mungu.


Yeye huzikata roho za wakuu; Na kuwatisha wafalme wa dunia.


BWANA, Mungu wa majeshi, Ni nani aliye hodari kama Wewe, Ee YAHU? Na uaminifu wako unakuzunguka.


BWANA ametamalaki, amejivika adhama, BWANA amejivika, ukuu na nguvu, kama mavazi ya kifalme. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;


Upepo wa kusi huleta mvua; Vile vile asingiziaye huleta uso wa ghadhabu.


Ingia ndani ya jabali; ukajifiche mavumbini mbele za utisho wa BWANA, mbele za utukufu wa enzi yake.


Na watu wataingia ndani ya pango za majabali, na ndani ya mashimo ya nchi, mbele za utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia.


Naye atasimama, na kulisha kundi lake kwa nguvu za BWANA, kwa enzi ya jina la BWANA, Mungu wake; nao watakaa; maana sasa atakuwa mkuu hadi miisho ya dunia.


BWANA si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; BWANA ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.


Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wa Mungu na chapa kamili ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi katika mkono wa kulia wa Ukuu huko juu;


maana Mungu wetu ni moto ulao.


Yeye aliye Mungu pekee, Mwokozi wetu kwa Yesu Kristo Bwana wetu; utukufu una yeye, na ukuu, na uwezo, na nguvu, tangu milele, na sasa, na hata milele. Amina.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo