Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 37:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Nalo hugeuzwa huku na huku kwa uongozi wake, Ili yafanye yote atakayoyaagiza Juu ya uso wa dunia hii ikaayo watu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Kwa amri yake vyote huzunguka huku na huko, kutekeleza kila kitu anachokiamuru, kufanyika katika ulimwengu wa viumbe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Kwa amri yake vyote huzunguka huku na huko, kutekeleza kila kitu anachokiamuru, kufanyika katika ulimwengu wa viumbe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Kwa amri yake vyote huzunguka huku na huko, kutekeleza kila kitu anachokiamuru, kufanyika katika ulimwengu wa viumbe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Nayo mawingu huzungukazunguka pande zote kwa amri yake, juu ya uso wa dunia yote, kufanya lolote ayaamuruyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Nayo mawingu huzungukazunguka pande zote kwa amri yake, juu ya uso wa dunia yote, kufanya lolote ayaamuruyo.

Tazama sura Nakili




Yobu 37:12
13 Marejeleo ya Msalaba  

Yeye huifunika mikono yake kwa umeme; Na kuuagiza shabaha utakayopiga.


Yeye huituma iende chini ya mbingu zote, Na radi yake hata miisho ya nchi.


Ee BWANA, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. Dunia imejaa viumbe wako.


Huipeleka amri yake juu ya nchi, Neno lake lapiga mbio sana.


Moto na mvua ya mawe, theluji na mvuke, Upepo wa dhoruba utimizao neno lake.


Fanyeni tayari machinjo kwa watoto wake. Kwa sababu ya uovu wa baba zao; Wasije wakainuka na kuitamalaki nchi, Na kuujaza uso wa ulimwengu kwa miji.


Siku zijazo Yakobo atatia mizizi; Israeli atatoa maua na kuchipuka; Nao watajaza uso wa ulimwengu matunda.


Je! Katika vitu vya ubatili vya mataifa, kiko kitu kiwezacho kuleta mvua? Je! Mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je! Si wewe, Ee BWANA, Mungu wetu? Kwa sababu hiyo tutakungoja; kwa kuwa wewe umevifanya vitu hivi vyote.


Furahini, basi, enyi wana wa Sayuni, mkamfurahie BWANA, Mungu wenu; kwa kuwa yeye huwapa ninyi mvua ya masika, kwa kipimo cha haki, naye huwanyeshea mvua, mvua ya masika, na mvua ya vuli, kama awali.


Tena nimeizuia mvua msiipate, ilipobaki miezi mitatu kabla ya mavuno; nami nimenyesha mvua juu ya mji mmoja, nikaizuia mvua isinyeshe juu ya mji mwingine; sehemu moja ilipata mvua, na sehemu isiyopata mvua ilikauka.


Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo