Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 34:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

29 Akitoa utulivu yeye, ni nani awezaye kuhukumia makosa? Akificha uso wake, ni nani awezaye kumtazama? Kama hufanyiwa taifa, au mtu mmoja, ni sawasawa;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Kama Mungu akinyamaza, nani awezaye kumlaumu? Kama akificha uso wake, nani awezaye kumwona,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Kama Mungu akinyamaza, nani awezaye kumlaumu? Kama akificha uso wake, nani awezaye kumwona,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Kama Mungu akinyamaza, nani awezaye kumlaumu? Kama akificha uso wake, nani awezaye kumwona,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Lakini akikaa kimya, ni nani awezaye kumhukumu? Akiuficha uso wake, ni nani awezaye kumwona? Ikiwa ni taifa au mtu mmoja, kwake ni sawa,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Lakini kama akinyamaza kimya, ni nani awezaye kumhukumu? Kama akiuficha uso wake, ni nani awezaye kumwona? Ikiwa ni taifa au mtu mmoja, kwake ni sawa,

Tazama sura Nakili




Yobu 34:29
26 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa, mfalme alipokuwa akikaa katika nyumba yake, hapo BWANA alipomstarehesha, asiudhiwe na adui zake waliomzunguka pande zote,


naam, kama ilivyokuwa tangu siku ile nilipowaamuru waamuzi, wawe juu ya watu wangu Israeli; nami nitakustarehesha mbele ya adui zako wote. Tena BWANA anakuambia ya kwamba BWANA atakujengea nyumba.


Basi ukatulia ufalme wake Yehoshafati; kwa sababu Mungu wake alimstarehesha pande zote.


Tazama, yuavunja, wala haiwezekani kujenga tena; Humfunga mtu, wala haiwezekani kumfungua.


Lakini yeye ni mmoja, ni nani awezaye kumgeuza? Tena nafsi yake ilitakalo, ndilo afanyalo.


Hata wakafanya kilio cha maskini kumfikia, Naye akasikia kilio cha hao wateswao.


Ili huyo mpotovu asitawale, Wala pasiwe na wa kuwatega watu.


Ee BWANA, utanisahau hadi lini, hata milele? Hadi lini utanificha uso wako?


Ee BWANA, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni.


Usinifiche uso wako, Usimkatalie mtumishi wako kwa hasira. Umekuwa msaada wangu, usinitupe, Wala usiniache, Ee Mungu wa wokovu wangu.


BWANA, kwa radhi yako Wewe uliuimarisha mlima wangu. Uliuficha uso wako, Nami nikafadhaika.


Awaadibuye mataifa, asikemee? Amfundishaye mwanadamu, asijue?


Ukimponya katika siku za shida, Hadi asiye haki atakapochimbiwa shimo.


Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.


Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.


Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima.


Na itakuwa, taifa lile na mfalme yule asiyetaka kumtumikia Nebukadneza, huyo mfalme wa Babeli, na kutia shingo zao katika nira ya mfalme wa Babeli, mimi nitaliadhibu taifa lile kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, asema BWANA, hata nitakapokuwa nimewaangamiza kwa mkono wake.


Mimi mwenyewe nitawalisha kondoo wangu, nami nitawalaza, asema Bwana MUNGU.


Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.


Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo