Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yobu 34:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 Kwani macho yake yako juu ya njia za mtu, Naye huziona hatua zake zote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 “Macho ya Mungu huchunguza mienendo ya watu; yeye huziona hatua zao zote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 “Macho ya Mungu huchunguza mienendo ya watu; yeye huziona hatua zao zote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 “Macho ya Mungu huchunguza mienendo ya watu; yeye huziona hatua zao zote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 “Macho yake yanazitazama njia za wanadamu; anaona kila hatua yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 “Macho yake yanazitazama njia za wanadamu; anaona kila hatua yao.

Tazama sura Nakili




Yobu 34:21
18 Marejeleo ya Msalaba  

Akampa jina BWANA aliyesema naye, “Wewe U Mungu uonaye,” kwani alisema, “Kweli nimemwona Mungu na nikaendelea kuishi baada ya kumuona?”


Kwa maana macho ya BWANA hukimbia kimbia duniani kote, ili ajionesha kuwa mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.


Je! Wewe una macho ya kimwili, Au je! Waona kama aonavyo binadamu?


Kwa kuwa yeye awajua watu baradhuli; Anapouona uovu, je; hatauangalia?


Hili nalo litakuwa ni wokovu wangu; Kwani asiyemcha Mungu hatakaribia mbele yake.


Lakini sasa wazihesabu hatua zangu; Je! Huchungulii dhambi yangu?


Huwapa usalama, nao wapumzika kwao; Na macho yake yako juu ya njia zao.


Je! Yeye hazioni njia zangu, Na kuzihesabu hatua zangu zote?


Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu;


Yeye aiumbaye mioyo yao wote Na kuziona kazi zao zote.


Macho ya BWANA huwaelekea wenye haki, Na masikio yake hukielekea kilio chao.


Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema.


Kwa maana njia za mwanadamu ziko mbele ya macho ya BWANA, Na mienendo yake yote huitafakari.


Maana macho yangu yaziangalia njia zao zote, hawakufichwa uso wangu usiwaone, wala haukusitirika uovu wao macho yangu yasiuone.


Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.


Je, mtu yeyote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema BWANA. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema BWANA.


mkuu wa mashauri, muweza katika kutenda; ambaye macho yake yamefumbuka juu ya njia zote za wanadamu, kumpa kila mtu kwa kadiri ya njia zake, na kwa kadiri ya matunda ya matendo yake,


Angalieni, macho ya Bwana MUNGU yanauangalia ufalme wenye dhambi, nami nitauangamiza utoke juu ya uso wa dunia; lakini sitaiangamiza kabisa nyumba ya Yakobo, asema BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo