Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 33:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

26 Yeye humwomba Mungu, naye akamtakabalia; Hata auone uso wake kwa furaha; Naye humrejeshea mtu haki yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Kisha atamwomba Mungu na kukubaliwa, atakuja mbele yake kwa furaha, na Mungu atamrudishia fahari yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Kisha atamwomba Mungu na kukubaliwa, atakuja mbele yake kwa furaha, na Mungu atamrudishia fahari yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Kisha atamwomba Mungu na kukubaliwa, atakuja mbele yake kwa furaha, na Mungu atamrudishia fahari yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Humwomba Mungu, akapata kibali kwake, huuona uso wa Mungu na kushangilia kwa furaha; Mungu humrudisha katika hali yake ya uadilifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Humwomba Mungu, akapata kibali kwake, huuona uso wa Mungu na kushangilia kwa furaha; Mungu humrudisha katika hali yake ya uadilifu.

Tazama sura Nakili




Yobu 33:26
35 Marejeleo ya Msalaba  

Sala yake pia, na jinsi Mungu alivyomtakabali, na dhambi yake yote, na kosa lake, na mahali alipopajenga mahali pa juu, na kupasimamishia Maashera na sanamu za kuchonga, kabla ya kujinyenyekeza; tazama, hayo yameandikwa katika Kumbukumbu ya Hozai.


Nami nitamwona mimi nafsi yangu, Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine. Mtima wangu unazimia ndani yangu!


Nyama ya mwili wake itakuwa laini kuliko ya mtoto; Huzirudia siku za ujana wake;


Kwani atamlipa binadamu kwa kazi yake, Naye atamfanya kila mtu kuona kulingana na njia zake.


Hata wakafanya kilio cha maskini kumfikia, Naye akasikia kilio cha hao wateswao.


Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako kuna furaha tele; Na katika mkono wako wa kulia Mna mema ya milele.


BWANA alinitendea sawasawa na haki yangu, Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa.


Na ahimidiwe BWANA. Maana ameisikia sauti ya dua yangu;


Maana ghadhabu zake ni za muda mfupi tu; Radhi yake ni ya milele. Kilio huweza kuwapo usiku, Lakini furaha huja asubuhi.


Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye Juu nadhiri zako.


Uniite siku ya mateso; Nitakuokoa, nawe utanitukuza.


Na fadhili ziko kwako, Ee Bwana; Maana ndiwe umlipaye kila mtu Kulingana na haki yake.


Mungu na atufadhili na kutubariki, Na kutuangazia uso wake.


Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;


Ukisema, Sisi hatukujua hayo; Je! Yeye aipimaye mioyo siye afahamuye? Naye ailindaye nafsi yako siye ajuaye? Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake?


Kwa maana watu watakaa katika Sayuni huko Yerusalemu; wewe hutalia tena; hakika yake atakuonea rehema nyingi kwa sauti ya kilio chako; asikiapo ndipo atakapokujibu.


Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.


Umenijulisha njia za uzima; Utanijaza furaha kwa uso wako.


Bwana akamwambia, Simama, nenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba;


akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo.


Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu;


BWANA humlipa kila mtu kulingana na haki na uaminifu wake; maana BWANA amekutia mikononi mwangu leo, nami nilikataa kuunyosha mkono wangu juu ya masihi wa BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo