Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 33:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

22 Naam, nafsi yake inakaribia shimoni, Na uhai wake unakaribia waangamizi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Yuko karibu sana kuingia kaburini, na maisha yake karibu na wale waletao kifo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Yuko karibu sana kuingia kaburini, na maisha yake karibu na wale waletao kifo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Yuko karibu sana kuingia kaburini, na maisha yake karibu na wale waletao kifo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Nafsi yake inakaribia kaburi, nao uhai wake karibu na wajumbe wa kifo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Nafsi yake inakaribia kaburi, nao uhai wake karibu na wajumbe wa kifo.

Tazama sura Nakili




Yobu 33:22
17 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini huyo malaika aliponyosha mkono wake kuelekea Yerusalemu ili auharibu, BWANA akaghairi katika mabaya, akamwambia huyo malaika mwenye kuwaharibu watu, Yatosha, sasa ulegeze mkono wako. Naye yule malaika wa BWANA alikuwako karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi.


Sauti za utisho zi masikioni mwake; Katika kufanikiwa kwake mtekaji nyara atamjia juu yake;


Roho yangu imezimia, siku zangu zimekoma, Kaburi i tayari kunipokea.


Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga.


Yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni, Na uhai wangu utautazama mwanga.


Kumbuka ya kwamba maisha yangu ni upepo; Jicho langu halitaona mema tena.


Nafsi zao zachukia kila namna ya chakula, Wameyakaribia malango ya mauti.


Kuhusu matendo ya wanadamu; Kwa neno la midomo yako Nimejiepusha na njia za wenye jeuri.


Umeniinua nafsi yangu, Ee BWANA, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao Shimoni.


Kwa kuwa BWANA atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, BWANA atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mharibifu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi.


Nilisema, Katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu; Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu.


Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na wadudu, akatokwa na roho.


Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakauawa na mharibifu.


Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kigiriki analo jina lake Apolioni.


BWANA huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hadi kuzimu, tena huleta juu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo