Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 33:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 “Mungu humrudi mtu kwa maumivu yamwekayo kitandani, maumivu hushika viungo vyake bila kukoma;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 “Mungu humrudi mtu kwa maumivu yamwekayo kitandani, maumivu hushika viungo vyake bila kukoma;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 “Mungu humrudi mtu kwa maumivu yamwekayo kitandani, maumivu hushika viungo vyake bila kukoma;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Mtu anaweza kutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, kwa dhiki za mfululizo katika mifupa yake,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Mtu anaweza kutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, kwa dhiki za mfululizo katika mifupa yake,

Tazama sura Nakili




Yobu 33:19
18 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo Asa akamkasirikia mwonaji, akamtia katika nyumba ya magandalo gerezani, maana amemghadhibikia kwa sababu ya neno hilo. Na wakati uleule Asa akatesa baadhi ya watu.


Katika mwaka wa thelathini na tisa wa kumiliki kwake, Asa akashikwa na ugonjwa wa miguu; ugonjwa wake ukazidi sana; lakini hakumtafuta BWANA katika ugonjwa wake, bali alitafuta msaada wa waganga.


Mifupa yake imejaa ujana wake, Lakini utalala nchi naye mavumbini.


Nami nilizivunja taya za wasio haki, Na kumpokonya mawindo katika meno yake.


Wakati wa usiku mifupa yangu huchomeka ndani yangu, Na maumivu yanayonitafuna hayapumziki.


Hapo nilalapo chini, nasema, Nitaondoka lini? Lakini usiku huwa mrefu; Nami nimejawa na kujitupa huku na huku hata kupambazuke.


Kabla sijateswa mimi nilipotea, Lakini sasa nimelitii neno lako.


Ilikuwa vema kwangu kuwa niliteswa, Nipate kujifunza amri zako.


Maana mchana kutwa nimepigwa, Na kuadhibiwa kila asubuhi.


Ee BWANA, heri mtu yule umwadibuye, Na kumfundisha kwa sheria yako;


Kwa maana kwa kila shauri kuna wakati na hukumu; kwa sababu mashaka ya mwanadamu yaliyo juu yake ni makubwa;


Basi, uovu wa Yakobo utatakaswa hivyo, na hayo ndiyo matunda yote ya kumwondolea dhambi yake; afanyapo mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa, hata maashera na sanamu za jua havitasimama tena.


Ila tuhukumiwapo, twarudiwa na Bwana, isije ikatupasa adhabu pamoja na dunia.


Nawe fikiri moyoni mwako, ya kuwa kama vile baba amrudivyo mwanawe, ndivyo BWANA, Mungu wako, akurudivyo.


Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo