Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yobu 33:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Kwa nini unapingana naye, ukisema, Hatajibu hata neno langu moja?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Kwa nini unashindana naye, ukisema hatajibu swali lako moja?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Kwa nini unashindana naye, ukisema hatajibu swali lako moja?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Kwa nini unashindana naye, ukisema hatajibu swali lako moja?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Kwa nini unamlalamikia kwamba yeye hamjibu mwanadamu?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Kwa nini unamlalamikia kwamba yeye hamjibu mwanadamu?

Tazama sura Nakili




Yobu 33:13
21 Marejeleo ya Msalaba  

Nitamwambia Mungu, Usinihukumie makosa; Nijulishe kwa nini unapingana nami.


Hata ukaulizauliza habari za uovu wangu, Na kuitafuta dhambi yangu,


Je! Wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu? Waweza kuufikia upeo wa huyo Mwenyezi?


Je! Mwenye hoja atashindana na Mwenyezi? Mwenye kujadiliana na Mungu, na ajibu yeye.


Tazama, yuanyakua, ni nani awezaye kumzuia? Ni nani awezaye kumwuliza, Wafanya nini?


Je! Mimi nitamjibuje, Na kuyachagua maneno yangu kuhojiana naye?


Mara moja amenena Mungu; Mara mbili nimeyasikia haya, Ya kuwa nguvu zina Mungu,


Ole wake ashindanaye na Muumba wake! Kigae kimoja katika vigae vya dunia! Je! Udongo umwambie yeye aufinyangaye; Unatengeneza nini? Au chombo ulichotengeneza hakina mikono?


nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.


Nimekutegea mtego, Ee Babeli, nawe ukanaswa, nawe ulikuwa huna habari; umeonekana, ukakamatwa, kwa sababu ulishindana na BWANA.


Je! Moyo wako waweza kuvumilia, au mkono wako waweza kuwa hodari, katika siku zile nitakapokutenda mambo? Mimi, BWANA, nimenena neno hili, tena nitalitenda.


na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe?


Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema?


Akawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe.


lakini ikiwa imetoka kwa Mungu hamwezi kuivunja; msije mkaonekana kuwa mnapigana na Mungu.


Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake?


La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwa nini umeniumba hivi?


Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?


Mambo ya siri ni ya BWANA, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo