Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 32:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 Lakini hakika imo roho ndani ya mwanadamu, Na pumzi ya Mwenyezi ndiyo impayo ufahamu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Lakini hiyo roho iliyomo ndani ya mtu, hiyo pumzi ya Mungu Mwenye Nguvu, ndio inayomwezesha mwanadamu kufahamu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Lakini hiyo roho iliyomo ndani ya mtu, hiyo pumzi ya Mungu Mwenye Nguvu, ndio inayomwezesha mwanadamu kufahamu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Lakini hiyo roho iliyomo ndani ya mtu, hiyo pumzi ya Mungu Mwenye Nguvu, ndio inayomwezesha mwanadamu kufahamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Lakini ni Roho iliyo ndani ya mwanadamu, pumzi ya Mwenyezi, ndiyo impayo ufahamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Lakini ni Roho iliyoko ndani ya mwanadamu, pumzi ya Mwenyezi, ndiyo impayo yeye ufahamu.

Tazama sura Nakili




Yobu 32:8
24 Marejeleo ya Msalaba  

Farao akawaambia watumishi wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye Roho ya Mungu ndani yake?


Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe.


basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.


Na Israeli wote wakapata habari za hukumu ile aliyoihukumu mfalme wakamwogopa mfalme; maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake, ili afanye hukumu.


Mungu akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani.


Watumishi wangu wataishusha toka Lebanoni mpaka baharini; nami nitaiendesha baharini, ikifungwa pamoja, mpaka mahali utakaponiagiza, huko nitaifungua ili wewe uichukue; ndivyo utakavyoitimiza haja yangu, ukiwapa chakula watu wa nyumbani mwangu.


Hekima na amri zina yeye [Mungu]; Yeye anayo ushauri na fahamu.


Kwake yeye ziko nguvu, na hekima; Huyo adanganywaye, na mdanganyi pia ni wake.


(Kwa kuwa uhai wangu ungali mzima ndani yangu, Na Roho ya Mungu iko katika pua yangu;)


Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia mhuri mafundisho yao,


Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.


Atufundishaye zaidi ya wanyama wa nchi, Na kutufanya wenye hekima kuliko ndege wa angani?


Je! Ni nani aliyetia hekima moyoni? Au ni nani aliyetia ufahamu rohoni?


Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;


Pumzi ya mwanadamu ni taa ya BWANA; Hupeleleza yote yaliyomo ndani yake.


Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.


Kwa maana Mungu wake anamwagiza vizuri na kumfundisha.


Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.


Yeye hubadili majira na nyakati; hutengua na kuteua wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa;


Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;


Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;


Lakini mmoja wenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo