Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yobu 32:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Tazama, tumbo langu ni kama divai iliyozibwa; Kama viriba vipya liko karibu kupasuka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Moyo wangu umefurika kama divai iliyozibwa, kama kiriba cha divai mpya tayari kupasuka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Moyo wangu umefurika kama divai iliyozibwa, kama kiriba cha divai mpya tayari kupasuka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Moyo wangu umefurika kama divai iliyozibwa, kama kiriba cha divai mpya tayari kupasuka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 ndani yangu niko kama chupa iliyojazwa divai, kama kiriba kipya cha divai kilicho karibu kupasuka.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 ndani yangu niko kama chupa iliyojazwa divai, kama kiriba kipya cha divai kilicho tayari kupasuka.

Tazama sura Nakili




Yobu 32:19
6 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa nimejaa maneno; Roho iliyo ndani yangu hunihimiza.


Nitanena, ili nipate kutulia; Nitafunua midomo yangu na kujibu.


Nami nikisema, Sitamtaja, wala sitasema tena kwa jina lake; basi, ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia.


Lakini nimejaa ghadhabu ya BWANA; nimechoka kwa kujizuia; imwageni juu ya watoto walio njiani, na juu ya kusanyiko la vijana pia; maana hata mume atatwaliwa pamoja na mkewe, mzee pamoja na yeye aliyetimiza siku zake.


Simba amekwisha kunguruma, ni nani asiyeogopa? Bwana MUNGU amenena, ni nani awezaye neno ila kutabiri?


Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama wakitia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, na viriba vikaharibika; bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo