Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 30:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Lakini sasa hao walio wadogo wangu hunifanyia mzaha, Ambao baba zao ningewadharau hata kuwasimamia mbwa wa kundi langu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 “Lakini sasa watu wananidhihaki, tena watu walio wadogo kuliko mimi; watu ambao baba zao niliwaona hawafai hata kuwaangalia mbwa wangu wakilinda kondoo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 “Lakini sasa watu wananidhihaki, tena watu walio wadogo kuliko mimi; watu ambao baba zao niliwaona hawafai hata kuwaangalia mbwa wangu wakilinda kondoo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 “Lakini sasa watu wananidhihaki, tena watu walio wadogo kuliko mimi; watu ambao baba zao niliwaona hawafai hata kuwaangalia mbwa wangu wakilinda kondoo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 “Lakini sasa watu wadogo kwa umri kuliko mimi wananidhihaki, watu ambao baba zao ningekataa kwa dharau kuwaweka pamoja na mbwa wangu wa kulinda kondoo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 “Lakini sasa watu wadogo kwa umri kuniliko wananidhihaki, watu ambao baba zao ningekataa kwa dharau kuwaweka pamoja na mbwa wangu wa kulinda kondoo.

Tazama sura Nakili




Yobu 30:1
17 Marejeleo ya Msalaba  

Akakwea kutoka huko mpaka Betheli; naye alipokuwa akienda njiani, wakatoka vijana katika mji, wakamfanyizia mzaha, wakamwambia, Paa wewe mwenye upaa! Paa wewe mwenye upaa!


Mimi ni mtu wa kuchekwa na jirani yake, Ni mtu niliyemwita Mungu, naye akanijibu; Huyo mwenye haki, aliye mtimilifu, amekuwa ni kicheko.


Naam, uwezo wa mikono yao utanifaa nini? Watu ambao nguvu zao zimekoma.


Wenye kiburi wamenidharau mno, Lakini sikiuki sheria zako.


Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za walevi hunidhihaki.


Nao watu wataonewa, kila mtu na mwenziwe, na kila mtu na jirani yake; mtoto atajivuna mbele ya mzee, na mtu mnyonge mbele ya mtu mwenye heshima.


Wengine wakaanza kumtemea mate, wakamfunika uso, na kumpiga makonde, na kumwambia, tabiri. Hata watumishi nao wakamchukua wakampiga makofi.


akawaambia, Mtu huyu mmemleta kwangu kana kwamba anapotosha watu; nami, tazama, nimeamua mambo yake mbele yenu, ila sikuona kwake kosa lolote katika mambo hayo mliyomshitaki;


Wakapiga kelele wote pamoja, wakisema, Mwondoe huyu, utufungulie Baraba.


Watu wakasimama wakitazama. Wale wakuu nao walikuwa wakimfanyia mzaha, wakisema, Aliokoa wengine; na ajiokoe mwenyewe, kama ndiye Kristo wa Mungu, mteule wake.


Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi.


Na Wayahudi wakaona wivu, wakajitwalia watu kadhaa miongoni mwa watu ovyo wasio na sifa njema, nao wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yasoni, wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji;


Mmoja wao, nabii wao wenyewe, amesema, Wakrete ni waongo siku zote, wanyama wabaya, walafi wavivu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo