Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 3:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

25 Maana jambo hilo nichalo hunipata, Nalo linitialo hofu hunijia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Kile ninachokiogopa kimenipata, ninachokihofia ndicho kilichonikumba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Kile ninachokiogopa kimenipata, ninachokihofia ndicho kilichonikumba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Kile ninachokiogopa kimenipata, ninachokihofia ndicho kilichonikumba.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Lile nililokuwa nikiogopa limenijia; lile nililokuwa nikihofia limenipata.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Lile nililokuwa naliogopa limenijia; lile nililokuwa ninalihofia limenipata.

Tazama sura Nakili




Yobu 3:25
6 Marejeleo ya Msalaba  

Basi ilikuwa, hapo hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Pengine hawa wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu sikuzote.


Vitisho vimenigeukia; Huifukuza heshima yangu kama upepo; Na kufanikiwa kwangu kumepita kama wingu.


Hapo nilipotazamia mema, ndipo yakaja mabaya; Nami nilipongojea mwanga, likaja giza.


Kwani msiba utokao kwa Mungu ulikuwa na kitisho kwangu, Na kwa sababu ya ukuu wake sikuweza kufanya neno.


Mimi ninayaogopa mateso yangu yote, Najua kuwa hutanihesabu kuwa sina hatia.


Ninyi mmeuogopa upanga; nami nitauleta upanga juu yenu, asema Bwana MUNGU.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo