Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 28:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

26 Hapo alipoiwekea mvua amri, Na njia kwa umeme wa radi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 alipoamua mvua inyeshe wapi, umeme na radi vipite wapi;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 alipoamua mvua inyeshe wapi, umeme na radi vipite wapi;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 alipoamua mvua inyeshe wapi, umeme na radi vipite wapi;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 alipofanya maagizo kwa ajili ya mvua na njia ya mwali wa radi,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 alipofanya maagizo kwa ajili ya mvua na njia kwa ajili ya umeme wa radi,

Tazama sura Nakili




Yobu 28:26
20 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo alipoiona na kuitangaza; Aliithibitisha, naam, na kuichunguza.


Tazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui; Hesabu ya miaka yake haichunguziki.


Maana yeye huvuta juu matone ya maji, Yamwagikayo katika mvua kutoka ukungu wake;


Naam, mtu aweza kuelewa matandazo ya mawingu, Ngurumo za makao yake?


Yeye huifunika mikono yake kwa umeme; Na kuuagiza shabaha utakayopiga.


Naam, huyatwika mawingu mazito mzigo wa maji; Hulitandika wingu la umeme wake;


Zisikizeni hizo kelele za sauti yake, Na uvumi utokao kinywani mwake.


Yeye huituma iende chini ya mbingu zote, Na radi yake hata miisho ya nchi.


Baadaye sauti hunguruma; Yeye hunguruma kwa sauti ya ukuu wake; Hazizuii hapo sauti yake isikiwapo.


Kwa kuwa huiambia theluji, Anguka juu ya nchi; Na pia kwa manyunyu ya mvua, Hayo manyunyu ya mvua yake nyingi.


Ni nani aliyepasua mfereji kwa maji ya gharika, Au njia kwa umeme wa radi;


Kunyesha mvua juu ya nchi isiyo na watu; Juu ya jangwa asiyokaa mwanadamu;


Kuishibisha nchi iliyo kame na ukiwa, Na kuyameza majani yaliyo mororo?


Ndiye apandishaye mvuke toka miisho ya nchi; Huifanyia mvua umeme; Hutoa upepo katika ghala zake.


Moto na mvua ya mawe, theluji na mvuke, Upepo wa dhoruba utimizao neno lake.


BWANA alikuwa nami katika mwanzo wa njia yake, Kabla ya matendo yake ya kale.


Je! Katika vitu vya ubatili vya mataifa, kiko kitu kiwezacho kuleta mvua? Je! Mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je! Si wewe, Ee BWANA, Mungu wetu? Kwa sababu hiyo tutakungoja; kwa kuwa wewe umevifanya vitu hivi vyote.


Tena nimeizuia mvua msiipate, ilipobaki miezi mitatu kabla ya mavuno; nami nimenyesha mvua juu ya mji mmoja, nikaizuia mvua isinyeshe juu ya mji mwingine; sehemu moja ilipata mvua, na sehemu isiyopata mvua ilikauka.


Mwombeni BWANA mvua wakati wa masika, naam, BWANA aletaye mawingu ya mvua, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi shambani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo