Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 27:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 Haki yangu naishika sana, wala sitaiacha; Moyo wangu hautanisuta wakati nikiwapo hai.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Nashikilia unyofu wangu, wala sitauacha; katika dhamiri yangu sina cha kunihukumu maishani mwangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Nashikilia unyofu wangu, wala sitauacha; katika dhamiri yangu sina cha kunihukumu maishani mwangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Nashikilia unyofu wangu, wala sitauacha; katika dhamiri yangu sina cha kunihukumu maishani mwangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Nitadumisha haki yangu wala sitaiacha; dhamiri yangu haitanisuta muda wote ninaoishi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Nitadumisha haki yangu wala sitaiacha; dhamiri yangu haitanisuta muda wote ninaoishi.

Tazama sura Nakili




Yobu 27:6
16 Marejeleo ya Msalaba  

Angalieni sasa, nimekwisha kulitengeneza neno langu, Najua ya kuwa mimi ni mwenye haki.


Lakini mwenye haki ataishika njia yake, Naye mwenye mikono safi atazidi kupata nguvu.


BWANA akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ijapokuwa ulinichochea juu yake, ili nimwangamize pasipokuwa na sababu.


Adui yangu na awe kama huyo mwovu, Na mpinzani wangu awe kama asiye haki.


Nilijivika haki, ikanifunika, Adili yangu ilikuwa kama joho na kilemba.


(Na nipimwe katika mizani iliyo sawasawa, Ili Mungu aujue uelekevu wangu);


Kwamba hatua yangu imekengeuka na kuiacha njia, Na moyo wangu kuyaandama macho yangu, Tena kwamba kipaku chochote kimeshikamana na mikono yangu;


Basi hao watu watatu wakaacha kumjibu Ayubu, kwa sababu alikuwa mwenye haki machoni pake mwenyewe.


Ndipo zikawaka hasira za huyo Elihu mwana wa Barakeli, Mbuzi, katika jamaa ya Ramu, juu ya Ayubu, kwa sababu alikuwa amejipa haki mwenyewe zaidi ya Mungu.


Je! Hata hukumu yangu utaibatilisha? Utanitia mimi hatiani, upate kuhesabiwa haki?


Rudini, nawasihi, lisiwe neno la udhalimu; Naam, rudini tena, neno langu ni la haki.


Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.


Nami ninajizoeza katika neno hili niwe na dhamiri isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele ya watu siku zote.


Nimekuwa mpumbavu, ninyi mmenilazimisha. Maana ilinipasa nisifiwe na ninyi; kwa sababu sikuwa duni ya mitume walio wakuu kwa lolote, nijapokuwa si kitu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo