Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 27:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Yumkini kuyatengeza, lakini wenye haki watayavaa, Nao wasio na hatia watazigawanya hizo fedha.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 na arundike tu, lakini mnyofu ndiye atakayeyavaa, na fedha yake watagawana watu wasio na hatia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 na arundike tu, lakini mnyofu ndiye atakayeyavaa, na fedha yake watagawana watu wasio na hatia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 na arundike tu, lakini mnyofu ndiye atakayeyavaa, na fedha yake watagawana watu wasio na hatia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa, naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa, naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake.

Tazama sura Nakili




Yobu 27:17
10 Marejeleo ya Msalaba  

Siku ile mfalme Ahasuero alimpa malkia Esta nyumba yake Hamani, yule adui ya Wayahudi. Mordekai naye akaja mbele ya mfalme; kwa maana Esta alikuwa amedhihirisha alivyomhusu.


Hatakuwa tajiri, wala mali zake hazitadumu, Wala mavuno yao hayatainama nchi.


Watoto wake watataka fadhili kwa maskini, Na mikono yake itarudisha mali yake.


Aliyoyataabikia kazi atayarudisha, asiyameze; Kwa mali aliyoyapata, hatafurahi.


Ajapokusanya fedha kama mavumbi, Na kujifanyia mavazi kama udongo kwa wingi;


Au pamoja na wakuu wenye dhahabu, Waliozijaza nyumba zao fedha;


Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.


Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.


Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.


Haya! Lieni, ninyi mkaao katika Makteshi, maana wafanya biashara wote wameangamia; hao wote wapimao fedha wamekatiliwa mbali.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo