Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 27:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

16 Ajapokusanya fedha kama mavumbi, Na kujifanyia mavazi kama udongo kwa wingi;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Hata akirundika fedha kama mavumbi, na mavazi kama udongo wa mfinyanzi,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Hata akirundika fedha kama mavumbi, na mavazi kama udongo wa mfinyanzi,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Hata akirundika fedha kama mavumbi, na mavazi kama udongo wa mfinyanzi,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi, na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi, na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi,

Tazama sura Nakili




Yobu 27:16
15 Marejeleo ya Msalaba  

Mfalme akafanya fedha humo Yerusalemu kuwa kama mawe, na mierezi akaifinya kuwa kama mikuyu iliyomo Shefela, kwa kuwa mingi.


Siku ile mfalme Ahasuero alimpa malkia Esta nyumba yake Hamani, yule adui ya Wayahudi. Mordekai naye akaja mbele ya mfalme; kwa maana Esta alikuwa amedhihirisha alivyomhusu.


Hatakuwa tajiri, wala mali zake hazitadumu, Wala mavuno yao hayatainama nchi.


Watoto wake watataka fadhili kwa maskini, Na mikono yake itarudisha mali yake.


Nawe hazina zako ziweke mchangani, Na dhahabu ya Ofiri iweke kati ya mawe ya vijito;


Hao watakaosalia kwake watakufa kwa maradhi mabaya, Wala wajane wake waliofiwa na waume hawataomboleza.


Yumkini kuyatengeza, lakini wenye haki watayavaa, Nao wasio na hatia watazigawanya hizo fedha.


Au pamoja na wakuu wenye dhahabu, Waliozijaza nyumba zao fedha;


Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.


Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.


Je! Hawa wote hawatapiga mfano juu yake, na mithali ya kusimanga juu yake, wakisema, Ole wake yeye aongezaye kisicho mali yake! Hata lini? Na ole wake yeye ajitwikaye mzigo wa rehani!


Haya! Lieni, ninyi mkaao katika Makteshi, maana wafanya biashara wote wameangamia; hao wote wapimao fedha wamekatiliwa mbali.


Na Tiro alijijengea ngome, akakusanya fedha kama mchanga, dhahabu safi kama matope ya njia kuu.


Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wezi huvunja na kuiba;


Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo