Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 24:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Watu huugua toka mji ulio na watu wengi, Na roho yake aliyejeruhiwa hupiga ukelele; Wala Mungu hauangalii upumbavu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Kutoka mjini kilio cha wanaokufa chasikika, na walioumizwa hupaza sauti kuomba msaada; lakini Mungu hasikilizi kabisa sala zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Kutoka mjini kilio cha wanaokufa chasikika, na walioumizwa hupaza sauti kuomba msaada; lakini Mungu hasikilizi kabisa sala zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Kutoka mjini kilio cha wanaokufa chasikika, na walioumizwa hupaza sauti kuomba msaada; lakini Mungu hasikilizi kabisa sala zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Kilio cha huzuni cha wanaokufa kinapaa kutoka mjini, nazo nafsi za waliojeruhiwa zinalilia msaada. Lakini Mungu hamlaumu mtu yeyote kwa kutenda mabaya.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Kilio cha huzuni cha wanaokufa kinapaa kutoka mjini, nazo nafsi za waliojeruhiwa zinalilia msaada. Lakini Mungu hamlaumu mtu yeyote kwa kutenda mabaya.

Tazama sura Nakili




Yobu 24:12
23 Marejeleo ya Msalaba  

Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.


Hushindika mafuta ndani ya kuta za watu hao; Wakanyaga mashinikizo, nao wana kiu.


Hawa ni katika hao waliouasi mwanga; Hawazijui njia zake, Wala hawakai katika mapito yake.


Kama hilo pigo likiua ghafla, Atayadhihaki majaribu yake asiye na kosa.


Dunia imetiwa mkononi mwa waovu; Yeye hufunika nyuso za waamuzi wake; Kama si yeye, ni nani basi?


Kwa nini mdhalimu amdharau Mungu. Akisema moyoni mwake, Hutapatiliza?


Kwa maana mimi ni mnyonge na mhitaji, Na moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu.


Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.


Ndivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza; Ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe. Lakini nitakukemea; Nitakuhukumu kwa hayo yote.


Maana wanamwudhi mtu uliyempiga Wewe, Wanazidisha maumivu ya hao uliowatia jeraha.


maana hiyo nguo ni kifuniko chake, hiyo peke yake ni nguo ya ngozi yake; je! Atalalia nini? Itakuwa, hapo atakaponililia mimi, nitasikia; kwa kuwa mimi ni mwenye rehema.


Kisha nikarudi na kuona udhalimu wote unaotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, lakini wale walikuwa hawana mfariji.


Basi sasa, nafanya nini hapa, asema BWANA, ikiwa watu wangu wamechukuliwa bure? Hao wanaowatawala wanapiga yowe, asema BWANA, na jina langu linatukanwa daima mchana kutwa.


Wewe u mwenye haki, Ee BWANA, nitetapo nawe, lakini nitasema nawe katika habari ya haki. Mbona njia ya wabaya inasitawi? Mbona wote watendao hila wanakaa salama?


Umewapanda, naam, wametia mizizi, wanakua, naam, wanazaa matunda; katika vinywa vyao u karibu, bali katika mioyo yao u mbali.


Mmemchokesha BWANA kwa maneno yenu. Lakini ninyi mwasema, Tumemchokesha kwa maneno gani? Kwa kuwa mwasema, Kila atendaye mabaya ni mwema machoni pa BWANA, naye huwafurahia watu hao, au, Mungu mwenye haki yuko wapi?


Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao.


Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;


Nao wakaiondoa hiyo miungu ya kigeni iliyokuwa kati yao, nao wakamtumikia BWANA; na roho yake ilihuzunika kwa sababu ya msiba wa Israeli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo