Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 16:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 Amenirarua katika ghadhabu zake, na kunionea; Amesagasaga meno juu yangu; Mtesi wangu hunikazia macho makali.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Amenirarua kwa hasira na kunichukia; amenisagia meno; na adui yangu ananikodolea macho.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Amenirarua kwa hasira na kunichukia; amenisagia meno; na adui yangu ananikodolea macho.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Amenirarua kwa hasira na kunichukia; amenisagia meno; na adui yangu ananikodolea macho.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Mungu amenishambulia na kunirarua katika hasira yake, na kunisagia meno yake; adui yangu hunikazia macho yake makali.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Mungu amenishambulia na kunirarua katika hasira yake, na kunisagia meno yake; adui yangu hunikazia macho yake makali.

Tazama sura Nakili




Yobu 16:9
17 Marejeleo ya Msalaba  

Mbona umeuficha uso wako, Na kunihesabu kuwa ni adui yako?


Waitia miguu yangu katika mkatale, na kuyakagua mapito yangu yote; Wajiandikia alama kuzizunguka nyayo za miguu yangu;


Wewe ujiraruaye mwenyewe katika hasira yako, Je! Dunia itaachwa kwa ajili yako wewe? Au jabali litaondolewa mahali pake?


Tena ameziwasha ghadhabu zake juu yangu, Akanihesabia kuwa mmoja katika watesi wake.


Wewe umegeuka kuwa mkali kwangu; Nawe waniudhi kwa uweza wa mkono wako.


Tazama, yuaona sababu za kufarakana nami, Hunihesabu kuwa ni adui yake;


Kwa kuwa mishale ya huyo Mwenyezi iko ndani yangu, Na roho yangu inainywa sumu yake; Vitisho vya Mungu vimejipanga juu yangu.


Bila heshima walinidhihaki kupindukia, Wakanisagia meno yao.


Asiye haki hunuia mabaya juu ya mwenye haki, Na kumsagia meno yake.


Yafahamuni hayo, Ninyi mnaomsahau Mungu, Nisije nikawararueni, Asipatikane wa kuwaokoa.


Juu yako adui zako wote Wamepanua vinywa vyao; Huzomea, husaga meno yao, Husema, Tumemmeza; Hakika siku hii ndiyo tuliyoitazamia; Tumeipata, tumeiona.


Alivyo kwangu ni kama dubu aoteaye, Kama simba aliye mafichoni.


Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efraimu, na kama mwanasimba kwa nyumba ya Yuda; mimi, naam, mimi nitararua, kisha nitakwenda zangu; nitachukua mbali, wala hapatakuwa na mtu wa kuokoa.


Njooni, tumrudie BWANA; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga majeraha yetu.


Usifurahi juu yangu, Ee adui yangu; niangukapo, nitasimama tena; nikaapo gizani, BWANA atakuwa nuru kwangu.


Basi waliposikia maneno haya, wakachomwa mioyo, wakamsagia meno.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo