Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yobu 16:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Mungu amenitia kwa hao wapotovu, Na kunitupa mikononi mwao waovu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Mungu amenitia mikononi mwa wajeuri, na kunitupa mikononi mwa waovu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Mungu amenitia mikononi mwa wajeuri, na kunitupa mikononi mwa waovu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Mungu amenitia mikononi mwa wajeuri, na kunitupa mikononi mwa waovu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Mungu amenigeuzia kwa watu wapotovu, na kunitupa katika makucha ya waovu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Mungu amenigeuzia kwa watu wabaya, na kunitupa katika makucha ya waovu.

Tazama sura Nakili




Yobu 16:11
17 Marejeleo ya Msalaba  

Je! Ni vema kwako wewe kuonea, Na kuidharau kazi ya mikono yako, Na kuiunga mkono mipango ya waovu?


Wamenifumbulia vinywa vyao; Wamenipiga shavuni kwa kunitukana; Hukutana pamoja juu yangu.


Nilikuwa katika raha, naye akanivunjavunja; Naam, amenishika shingo, na kuniponda; Tena amenisimamisha niwe shabaha yake.


Mbona ninyi mnaniudhi kama Mungu, Wala hamkutosheka na nyama yangu?


Jueni basi kuwa Mungu amenipotosha, Na kunizingira kwa wavu wake.


Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA, akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hadi utosi wa kichwa.


Kama aishivyo Mungu, aliyeniondolea haki yangu; Huyo Mwenyezi aliyeitesa nafsi yangu;


Je! Hata hukumu yangu utaibatilisha? Utanitia mimi hatiani, upate kuhesabiwa haki?


Dunia imetiwa mkononi mwa waovu; Yeye hufunika nyuso za waamuzi wake; Kama si yeye, ni nani basi?


Usinitie katika nia ya watesi wangu; Maana mashahidi wa uongo wamenijia, Nao watoao jeuri kama pumzi.


Wala hukunitia mikononi mwa adui; Miguu yangu umeisimamisha mahali penye usalama.


Tazama, huyu ametunga uovu, Amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo.


Basi ndipo alipomtia mikononi mwao ili asulubiwe; nao wakampokea Yesu.


Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.


Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nilipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.


Nawe umeonesha leo jinsi ulivyonitendea mema, kwani BWANA aliponitia mikononi mwako, hukuniua.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo