Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 12:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 Hema za wanyang'anyi hufanikiwa, Na hao wamkasirishao Mungu hukaa salama; Mikononi mwao Mungu huleta vitu vingi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Makao ya wanyanganyi yana amani; wenye kumchokoza Mungu wako salama, nguvu yao ni mungu wao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Makao ya wanyanganyi yana amani; wenye kumchokoza Mungu wako salama, nguvu yao ni mungu wao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Makao ya wanyang'anyi yana amani; wenye kumchokoza Mungu wako salama, nguvu yao ni mungu wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Mahema ya wanyang’anyi hayasumbuliwi, wale wanaomghadhibisha Mungu wako salama: wale wamchukuao mungu wao mikononi mwao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Hema za wanyang’anyi hazisumbuliwi, wale wanaomghadhibisha Mungu wako salama: wale wamchukuao mungu wao mikononi mwao.

Tazama sura Nakili




Yobu 12:6
17 Marejeleo ya Msalaba  

Katika mawazo yake huyo aliye na raha mna kudharau balaa; Tayari kwa ajili ya wenye kuteleza miguu.


Lakini sasa waulize hao wanyama, nao watakufundisha; Na ndege wa angani, nao watakuambia;


Hata ukageuza roho yako kinyume cha Mungu, Na kuyatoa maneno kama hayo kinywani mwako.


Naye ndiye aliyezijaza nyumba zao vitu vyema; Lakini mashauri ya waovu na yawe mbali nami.


Huwapa usalama, nao wapumzika kwao; Na macho yake yako juu ya njia zao.


Dunia imetiwa mkononi mwa waovu; Yeye hufunika nyuso za waamuzi wake; Kama si yeye, ni nani basi?


Ee BWANA, kwa mkono wako uniokoe na watu, Watu wa dunia hii ambao fungu lao liko katika maisha haya. Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako, Hushiba wana, huwaachia watoto wao akiba zao,


Usihangaike kwa sababu ya watenda mabaya, Usiwahusudu wafanyao ubatili.


Nimemwona mtu asiye haki mkali sana, Akijieneza kama mwerezi wa Lebanoni.


Maana niliwaonea wivu wenye kujivuna, Nilipoiona hali ya amani ya wasio haki.


Hata wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakastawi. Mwishowe wataangamizwa milele;


Wewe u mwenye haki, Ee BWANA, nitetapo nawe, lakini nitasema nawe katika habari ya haki. Mbona njia ya wabaya inasitawi? Mbona wote watendao hila wanakaa salama?


Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa wakuu, wamepata mali.


Wamenenepa sana, wang'aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji.


Kisha atapita kwa kasi, kama upepo, atapita na kuwa ana hatia; yeye ambaye nguvu zake ni mungu wake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo