Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 12:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Yeye huwaondoa makuhani wakiwa wamevuliwa nguo. Na kuwapindua mashujaa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Huwaacha makuhani waende uchi; na kuwaangusha wenye nguvu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Huwaacha makuhani waende uchi; na kuwaangusha wenye nguvu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Huwaacha makuhani waende uchi; na kuwaangusha wenye nguvu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Huwaondoa makuhani wakiwa wametekwa nyara, na kuwaangusha waliojiimarisha muda mrefu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Huwaondoa makuhani wakiwa wametekwa nyara, na kuwaangusha waliojiimarisha muda mrefu.

Tazama sura Nakili




Yobu 12:19
16 Marejeleo ya Msalaba  

Amenivua utukufu wangu, Na kuiondoa taji kichwani mwangu.


Mbona waovu wanaishi, Na kuwa wazee, naam, na kuongezeka kuwa na nguvu?


Lakini huyo shujaa, nchi ilikuwa yake; Na huyo mwenye kusifiwa, yeye aliikaa.


Lakini Mungu huwadumisha wenye uwezo kwa nguvu zake; Huinuka, wasiokuwa na tumaini la kuishi.


Hufa ghafla, hata usiku wa manane; Watu hutikisika na kwenda zao, Nao mashujaa huondolewa pasipo mkono wa mtu.


Yeye huwavunjavunja mashujaa pasipo kuwachunguza, Na kuwaweka wengine mahali pao.


Hata wakafanya kilio cha maskini kumfikia, Naye akasikia kilio cha hao wateswao.


Kwa sababu ya wingi wa dhuluma wao hulia; Walilia msaada kwa sababu ya mkono wa wakuu.


ndiye awatanguaye wakuu, na kuwabatilisha waamuzi wa dunia.


Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kulia, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza nguvu za wafalme; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa.


Kisha ikawa hapo walipomletea Yoshua hao wafalme watano hapo nje, Yoshua akawaita wanaume wote wa Israeli, akawaambia majemadari wa watu wa vita waliokwenda naye, Haya, jongeeni karibu, mweke nyayo za miguu yenu katika shingo za wafalme hawa. Nao wakajongea karibu, wakatia nyayo zao katika shingo zao.


Na wafalme hao wote na nchi zao Yoshua akatwaa kwa wakati mmoja, kwa sababu yeye BWANA, Mungu wa Israeli, alipigana kwa ajili ya Israeli,


Hawa watafanya vita na Mwana-kondoo, na Mwana-kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo