Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 11:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Yeye akipita, na kufunga watu, Na kuwaita hukumuni, ni nani basi awezaye kumzuia?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Kama Mungu akipita, akamfunga mtu na kumhukumu, nani awezaye kumzuia?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Kama Mungu akipita, akamfunga mtu na kumhukumu, nani awezaye kumzuia?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Kama Mungu akipita, akamfunga mtu na kumhukumu, nani awezaye kumzuia?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 “Akija na kukufunga gerezani, na kuitisha mahakama, ni nani awezaye kumpinga?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 “Kama akija na kukufunga gerezani, na kuitisha mahakama, ni nani awezaye kumpinga?

Tazama sura Nakili




Yobu 11:10
13 Marejeleo ya Msalaba  

Cheo chake ni kirefu kuliko dunia, Ni kipana zaidi ya bahari.


Tazama, yuavunja, wala haiwezekani kujenga tena; Humfunga mtu, wala haiwezekani kumfungua.


Akitoa utulivu yeye, ni nani awezaye kuhukumia makosa? Akificha uso wake, ni nani awezaye kumtazama? Kama hufanyiwa taifa, au mtu mmoja, ni sawasawa;


Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango, Hapo ilipotoka kwa nguvu kama kwamba imetoka tumboni mwa nchi.


Kwani yeye huumiza, lakini tena huuguza; Yeye hutia jeraha, na mikono yake huponya.


Yeye ni mwenye hekima moyoni, na mwenye uwezo katika nguvu; Ni nani aliyejifanya kuwa mgumu juu yake, naye akafanikiwa?


Wala hukunitia mikononi mwa adui; Miguu yangu umeisimamisha mahali penye usalama.


Maana BWANA wa majeshi amekusudia, naye ni nani atakayelibatili? Na mkono wake ulionyoshwa, ni nani atakayeugeuza nyuma?


Mimi kwanza nitauambia Sayuni, Tazama; hawa ndio; nami nitampa Yerusalemu mletaji wa habari njema.


na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe?


Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama BWANA asingaliwatoa?


Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo