Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yobu 10:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 Kabla sijaenda huko ambako sitarudi kutoka huko tena, Ni hiyo nchi ya giza, giza tupu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 kabla ya kwenda huko ambako sitarudi, huko kwenye nchi ya huzuni na giza nene;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 kabla ya kwenda huko ambako sitarudi, huko kwenye nchi ya huzuni na giza nene;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 kabla ya kwenda huko ambako sitarudi, huko kwenye nchi ya huzuni na giza nene;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 kabla sijaenda mahali ambapo hakuna kurudi tena, katika nchi ya giza na uvuli wa mauti,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 kabla sijaenda mahali ambapo hakuna kurudi tena, katika nchi ya giza na uvuli wa mauti,

Tazama sura Nakili




Yobu 10:21
21 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini sasa amekufa nifungie nini? Je! Naweza kumrudisha tena? Mimi nitakwenda kwake lakini yeye hatanirudia mimi.


Kwa kuwa hatuna budi kufa, nasi tu kama maji yaliyomwagika chini, yasiyoweza kuzoleka tena; wala Mungu haondoi maisha ila hufikiri shauri, kwamba yeye aliyefukuzwa asiwe mkimbizi kwake.


Ni nchi ya giza kuu, kama giza lenyewe lilivyo; Ni nchi ya giza tupu, isiyo na mpango wowote wa mambo, Nchi ambayo nuru yake ni kama giza.


Kwani ikiisha pita miaka michache, Nitakwenda njia hiyo ambayo sitarudi tena.


Nikitazamia kuzimu kuwa nyumba yangu; Nikitandika malazi yangu gizani;


Maana hapo ningelala na kutulia; Ningelala usingizi; na kupata kupumzika;


Ishikwe na giza, giza tupu, kuwa yake; Wingu na likae juu yake; Chote kiifanyacho siku kuwa giza na kiitishe.


Hapana hofu ya giza kuu, mahali wawezapo kujificha watendao udhalimu.


Je! Umefunuliwa malango ya mauti, Au umeyaona malango ya kuzimu?


Naam, nijapopita kati ya bonde la kivuli cha mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.


Uache kunitazama, ndio nipate kufurahi tena, Kabla sijafa na kutoweka kabisa.


Mwanadamu mwenye heshima, iwapo hana akili, Amefanana na wanyama wapoteao.


Lakini mimi nimekulilia Wewe, BWANA, Na asubuhi maombi yangu yatakuwasilia.


Mimi umenilaza chini katika shimo, Katika mahali penye giza vilindini.


Naam, mtu akiishi miaka mingi, na aifurahie yote; lakini na azikumbuke siku zijazo za giza, kwa maana zitakuwa nyingi. Mambo yote yajayo ni ubatili.


Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.


Nilisema, Sitamwona BWANA, yeye BWANA, katika nchi ya walio hai; Sitamwona mwanadamu tena pamoja na hao wakaao duniani.


Wala hawakusema, Yuko wapi BWANA, aliyetutoa katika nchi ya Misri; akatuongoza jangwani, katika nchi ya ukame na mashimo, katika nchi ya kiu na ya kivuli cha mauti, katika nchi ambayo ndani yake hapiti mtu, wala haikukaliwa na watu?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo