Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yobu 1:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

7 BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzungukazunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Mwenyezi-Mungu akamwuliza Shetani, “Umetoka wapi wewe?” Naye Shetani akamjibu Mwenyezi-Mungu, “Nimetoka kutembeatembea na kuzungukazunguka duniani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Mwenyezi-Mungu akamwuliza Shetani, “Umetoka wapi wewe?” Naye Shetani akamjibu Mwenyezi-Mungu, “Nimetoka kutembeatembea na kuzungukazunguka duniani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Mwenyezi-Mungu akamwuliza Shetani, “Umetoka wapi wewe?” Naye Shetani akamjibu Mwenyezi-Mungu, “Nimetoka kutembeatembea na kuzungukazunguka duniani.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Mwenyezi Mungu akamwambia Shetani, “Umetoka wapi?” Shetani akamjibu Mwenyezi Mungu, “Natoka kuzunguka duniani, nikitembea huku na huko.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 bwana akamwambia Shetani, “Umetoka wapi?” Shetani akamjibu bwana, “Natoka kuzunguka pote duniani, nikitembea huku na huko humo.”

Tazama sura Nakili




Yobu 1:7
9 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini yeye akaingia, akasimama mbele ya bwana wake. Elisha akamwambia, Watoka wapi, Gehazi? Akanena, Mtumwa wako hakuenda mahali.


BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi? Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzungukazunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.


Farasi wale walipotoka, walitaka kwenda huku na huko katika dunia; naye akawaambia, Haya! Tokeni, mwende huku na huko katika dunia. Basi wakaenda huku na huko katika dunia.


Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.


Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze.


Lile joka kuu likatupwa, yule nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika wake wakatupwa pamoja naye.


naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo