Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 9:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

25 Tazama, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapowaadhibu wote waliotahiriwa katika hali yao ya kutotahiriwa;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Mwenyezi-Mungu asema: “Siku zaja ambapo nitawaadhibu wote waliotahiriwa mwilini tu:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Mwenyezi-Mungu asema: “Siku zaja ambapo nitawaadhibu wote waliotahiriwa mwilini tu:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Mwenyezi-Mungu asema: “Siku zaja ambapo nitawaadhibu wote waliotahiriwa mwilini tu:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 “Siku zinakuja, nitakapowaadhibu wale wote ambao wametahiriwa kimwili tu, asema Mwenyezi Mungu,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 “Siku zinakuja, nitakapowaadhibu wale wote ambao wametahiriwa kimwili tu, asema bwana,

Tazama sura Nakili




Yeremia 9:25
17 Marejeleo ya Msalaba  

Dedani, na Tema, na Buzi, na watu wote wakatao denge;


Jitahirini kwa BWANA, mkayaondoe magovi ya mioyo yenu, enyi watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu; ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikawaka hata mtu asiweze kuizima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.


Na ngamia wao watakuwa mateka, na wingi wa makundi yao utakuwa nyara; nami nitawatawanya katika pande zote watu wale wanyoao denge; nami nitaleta msiba wao toka pande zao zote, asema BWANA.


Utakufa kifo cha hao wasiotahiriwa, kwa mikono ya wageni; kwa maana mimi nimenena neno hili, asema Bwana MUNGU.


Umefanana na nani, hivi katika utukufu na ukuu, kati ya miti ya Adeni? Lakini utashushwa pamoja na miti ya Adeni, hata pande za chini za nchi; utalala kati ya hao wasiotahiriwa; pamoja na hao waliouawa kwa upanga. Huyu ndiye Farao, na jamii yote ya watu wake, asema Bwana MUNGU.


kuwa mmewaingiza wageni, ambao mioyo yao haikutahiriwa, wala miili yao haikutahiriwa, wawe ndani ya patakatifu pangu, wapatie unajisi, naam, nyumba yangu, mtoapo sadaka ya chakula changu, mafuta na damu; nao wameyavunja maagano yangu, juu ya machukizo yenu yote.


Msinyoe denge pembe za vichwani, wala msiharibu pembe za ndevu zenu.


mimi nami nimewaendea kinyume, na kuwatia katika nchi ya adui zao; lakini hapo, kama mioyo yao isiyokuwa tohara ikinyenyekea, nao wakubali adhabu ya uovu wao;


Ni ninyi tu niliowajua katika jamaa zote zilizo duniani; kwa sababu hiyo nitawapatiliza ninyi maovu yenu yote.


Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili;


bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.


Basi, Yonathani akamwambia yule kijana aliyembebea silaha zake, Haya! Na twende tukavuke ngomeni mwa hao wasiotahiriwa; yamkini BWANA atatutendea kazi; kwa maana hakuna la kumzuia BWANA asiokoe, kama ni kwa wengi au kama ni kwa wachache.


Daudi akaongea na watu waliosimama karibu, akisema, Je! Atafanyiwaje yeye atakayemwua Mfilisti huyo, na kuwaondolea Israeli aibu hii? Maana Mfilisti huyu asiyetahiriwa ni nani hata awatukane majeshi ya Mungu aliye hai?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo