Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 9:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

23 BWANA asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Mwenye hekima asijivunie nguvu zake, wala tajiri asijivunie utajiri wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Mwenye hekima asijivunie nguvu zake, wala tajiri asijivunie utajiri wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Mwenye hekima asijivunie nguvu zake, wala tajiri asijivunie utajiri wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Mwenye hekima asijisifu katika hekima yake, au mwenye nguvu ajisifu katika nguvu zake, wala tajiri ajisifu katika utajiri wake,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Hili ndilo asemalo bwana: “Mwenye hekima asijisifu katika hekima yake, au mwenye nguvu ajisifu katika nguvu zake, wala tajiri ajisifu katika utajiri wake,

Tazama sura Nakili




Yeremia 9:23
54 Marejeleo ya Msalaba  

Jitunzeni msiseme, Sisi tumepata hekima; Mungu huenda akamshinda, si mtu;


Magamba yake yenye nguvu ndiyo fahari yake, Yamefungamana pamoja kama yaliyofungwa kwa mhuri.


Huzipenda haki na hukumu, Nchi imejaa fadhili za BWANA.


Mtukuzeni BWANA pamoja nami, Na tuliadhimishe jina lake pamoja.


Lakini umetutupa, umetufedhehesha, Wala huendi na majeshi yetu.


Msiitumainie dhuluma, Wala msijivune kwa unyang'anyi; Mali izidipo msiiangalie sana moyoni.


Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu; Bali haki huokoa na mauti.


Hapana hekima, wala ufahamu, Wala shauri, juu ya BWANA.


Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;


Naye ni nani ajuaye kama huyo atakuwa mwenye hekima au mpumbavu? Hata hivyo atatawala juu ya kazi yangu yote niliyojishughulisha nayo, ambamo ndani yake mimi nimeonesha hekima chini ya jua. Hayo nayo ni ubatili.


Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.


Maana asema, Je! Wakuu wangu si wote wafalme?


Nao watafadhaika, na kuona haya kwa ajili ya Kushi, matumaini yao, na Misri, utukufu wao.


Maana umeutumainia ubaya wako; umesema, Hapana anionaye; hekima yako, na maarifa yako yamekupotosha, nawe umesema moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi.


Ole wao walio na hekima katika macho yao wenyewe, na wenye busara katika fikira zao wenyewe!


Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue BWANA; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hadi aliye mkubwa miongoni mwao, asema BWANA; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.


Mwasemaje ninyi, Sisi tu mashujaa, watu hodari wa vita.


Maana, kwa kuwa umeyatumainia matendo yako, na hazina zako, wewe nawe utatwaliwa; na Kemoshi atatoka aende katika uhamisho, makuhani wake na wakuu wake pamoja.


Mbona unajisifu kwa sababu ya mabonde, bonde lako litiririkalo, Ee binti mwenye kuasi? Utumainiaye hazina zako, ukisema, Ni nani atakayenijia?


Nayo nchi ya Misri itakuwa ukiwa na jangwa; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA; kwa sababu amesema, Mto huu ni wangu, nami nimeufanya.


Watatupa fedha yao katika njia kuu za mji, na dhahabu yao itakuwa kama kitu cha unajisi; fedha yao na dhahabu yao hazitaweza kuwaokoa siku ya ghadhabu ya BWANA; hawatajishibisha roho zao, wala hawatajijaza matumbo yao; kwa sababu zilikuwa kwazo la uovu wao.


Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zumari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuri liwakalo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi mikononi mwangu?


Basi mimi, Nebukadneza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.


Ee mwanadamu, yeye amekuonesha yaliyo mema; na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!


Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya BWANA; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, mwisho wa kutisha.


Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, jinsi ilivyo shida wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu!


Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;


kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.


Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo.


ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake;


Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;


Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.


Hata Mfilisti alipotazama huku na huku, akamwona Daudi akamdharau; kwa kuwa ni kijana tu mwekundu, tena ana sura nzuri.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo