Yeremia 9:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC
22 Nena, BWANA asema hivi, Mizoga ya watu itaanguka kama samadi juu ya mashamba, Na kama konzi ya ngano nyuma yake avunaye, wala hapana mtu atakayeikusanya.
22 Maiti za watu zimetapakaa kila mahali kama marundo ya mavi mashambani, kama masuke yaliyoachwa na mvunaji, wala hakuna atakayeyakusanya.’ Ndivyo alivyoniambia Mwenyezi-Mungu niseme.”
22 Maiti za watu zimetapakaa kila mahali kama marundo ya mavi mashambani, kama masuke yaliyoachwa na mvunaji, wala hakuna atakayeyakusanya.’ Ndivyo alivyoniambia Mwenyezi-Mungu niseme.”
22 Maiti za watu zimetapakaa kila mahali kama marundo ya mavi mashambani, kama masuke yaliyoachwa na mvunaji, wala hakuna atakayeyakusanya.’ Ndivyo alivyoniambia Mwenyezi-Mungu niseme.”
22 Sema, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “ ‘Mizoga ya watu italala kama kinyesi katika mashamba, kama malundo ya nafaka nyuma ya mvunaji, wala hakuna atakayeikusanya.’ ”
22 Sema, “Hili ndilo asemalo bwana: “ ‘Maiti za wanaume zitalala kama mavi katika mashamba, kama malundo ya nafaka nyuma ya mvunaji, wala hakuna anayekusanya.’ ”
Hezekia akawasikiliza, akawaonesha nyumba yote yenye vitu vyake vya thamani, fedha, na dhahabu, na manukato, na marhamu ya thamani, na nyumba yenye silaha zake, na vitu vyote vilivyoonekana katika hazina zake. Wala hapakuwa na kitu asichowaonesha Hezekia, katika nyumba yake, wala katika ufalme wake wote.
Kwa sababu hiyo hasira ya BWANA imewaka juu ya watu wake, naye amenyosha mkono wake juu yao; akawapiga, navyo vilima vilitetemeka, na mizoga yao ilikuwa kama takataka katika njia kuu. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.
watakufa kwa maradhi mabaya; hawataliliwa, wala hawatazikwa; watakuwa kama samadi juu ya uso wa nchi; nao wataangamizwa kwa upanga, na kwa njaa; na mizoga yao itakuwa chakula cha ndege wa angani, na cha wanyama wa nchi.
Na waliouawa na BWANA siku ile watakuwapo, toka upande mmoja wa dunia hata upande wa pili; hawataliliwa, wala kukusanywa, wala kuzikwa; watakuwa samadi juu ya uso wa nchi.
Basi, kwa hiyo, BWANA asema hivi, Tazama, nitaweka makwazo mbele ya watu hawa, na baba na wana wao watajikwaa pamoja; jirani ya mtu na rafiki yake watapotea.
nao wataitawanya mbele ya jua, na mwezi, na jeshi lote la mbinguni, walivyovipenda, na kuvitumikia, na kuandamana navyo, na kuvitafuta, na kuviabudu haitakusanywa pamoja tena, wala kuzikwa; itakuwa ni samadi juu ya uso wa nchi.
Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda BWANA dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi.