Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 9:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 Kwa maana mauti imepandia madirishani mwetu, imeingia majumbani mwetu; Ipate kuwakatilia mbali watoto walio nje, na vijana katika njia kuu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 ‘Kifo kimepenya madirisha yetu, kimeingia ndani ya majumba yetu; kimewakatilia mbali watoto wetu barabarani, vijana wetu katika viwanja vya mji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 ‘Kifo kimepenya madirisha yetu, kimeingia ndani ya majumba yetu; kimewakatilia mbali watoto wetu barabarani, vijana wetu katika viwanja vya mji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 ‘Kifo kimepenya madirisha yetu, kimeingia ndani ya majumba yetu; kimewakatilia mbali watoto wetu barabarani, vijana wetu katika viwanja vya mji.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Mauti imeingia ndani kupitia madirishani, imeingia kwenye majumba yetu ya fahari; imewakatilia mbali watoto katika barabara na vijana wa kiume kutoka viwanja vya miji.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Mauti imeingia ndani kupitia madirishani, imeingia kwenye majumba yetu ya fahari; imewakatilia mbali watoto katika barabara na vijana waume kutoka viwanja vya miji.

Tazama sura Nakili




Yeremia 9:21
17 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa hiyo akaleta juu yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao kwa upanga nyumbani mwa patakatifu pao, asiwahurumie kijana wala mwanamwali, mzee wala mnyonge; akawatia wote mkononi mwake.


Hata vijana watazimia na kuchoka, na vijana wanaume wataanguka;


Nami nimewapepea kwa kipepeo katika malango ya nchi nimewaondolea watoto wao, nimewaharibu watu wangu; hata hivyo hawakurudi na kuziacha njia zao.


Kwa sababu hiyo, uwatoe watoto wao waone njaa, uwatoe nguvu za upanga ziwapate; wake zao wafiwe na watoto wao, na kufiwa na waume zao; wanaume wao wauawe, na vijana wao wapigwe kwa upanga vitani.


Basi, sasa, BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa nini mnafanya uovu huu mkubwa juu ya nafsi zenu wenyewe, kujikatilia mbali mwanamume na mwanamke, mtoto mchanga na anyonyaye, mtoke kati ya Yuda, msijiachie mtu abakiye;


Kwa sababu hiyo vijana wake wataanguka katika njia zake kuu, na watu wake wa vita, wote pia, watanyamazishwa katika siku hiyo, asema BWANA.


Lakini nimejaa ghadhabu ya BWANA; nimechoka kwa kujizuia; imwageni juu ya watoto walio njiani, na juu ya kusanyiko la vijana pia; maana hata mume atatwaliwa pamoja na mkewe, mzee pamoja na yeye aliyetimiza siku zake.


Basi, kwa hiyo, BWANA asema hivi, Tazama, nitaweka makwazo mbele ya watu hawa, na baba na wana wao watajikwaa pamoja; jirani ya mtu na rafiki yake watapotea.


Na mizoga ya watu hawa itakuwa chakula cha ndege wa angani, na cha wanyama wa nchi; wala hapana mtu atakayewafukuza.


nao wataitawanya mbele ya jua, na mwezi, na jeshi lote la mbinguni, walivyovipenda, na kuvitumikia, na kuandamana navyo, na kuvitafuta, na kuviabudu haitakusanywa pamoja tena, wala kuzikwa; itakuwa ni samadi juu ya uso wa nchi.


Huurukia mji; hupiga mbio juu ya ukuta; hupanda na kuingia ndani ya nyumba; huingia madirishani kama aingiavyo mwizi.


Bikira wa Israeli ameanguka; hatainuka tena; Ameangushwa katika nchi yake; hakuna mtu wa kumwinua.


Hata itakuwa, wakisalia wanaume kumi katika nyumba moja, watakufa.


Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda BWANA dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo