Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 9:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 na wafanye haraka na kutuombolezea, ili macho yetu yachuruzike machozi, na kope zetu zibubujike maji.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Waambieni: ‘Njoni hima mkaomboleze juu yetu, macho yetu yapate kuchuruzika machozi, na kope zetu zibubujike machozi kama maji.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Waambieni: ‘Njoni hima mkaomboleze juu yetu, macho yetu yapate kuchuruzika machozi, na kope zetu zibubujike machozi kama maji.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Waambieni: ‘Njoni hima mkaomboleze juu yetu, macho yetu yapate kuchuruzika machozi, na kope zetu zibubujike machozi kama maji.’”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Nao waje upesi waomboleze juu yetu, hadi macho yetu yatiririke machozi na kope zetu zibubujike maji.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Nao waje upesi na kutuombolezea, mpaka macho yetu yafurike machozi na vijito vya maji vitoke kwenye kope zetu.

Tazama sura Nakili




Yeremia 9:18
19 Marejeleo ya Msalaba  

Macho yangu yachuruzika mito ya machozi, Kwa sababu hawaitii sheria yako.


Kwa sababu hiyo nasema, Geuza uso wako usinitazame, nipate kulia kwa uchungu; usijishughulishe kunifariji, kwa ajili ya kuharibika kwake binti ya watu wangu.


Bali kama hamtaki kusikia, roho yangu italia kwa siri, kwa sababu ya kiburi chenu; na jicho langu litalia sana na kutoka machozi mengi, kwa kuwa kundi la BWANA limechukuliwa mateka.


Nawe utawaambia neno hili, Macho yangu na yatiririke machozi, usiku na mchana, wala yasikome; kwa maana bikira, binti ya watu wangu, amevunjika mavunjiko makuu, kwa jeraha lisiloponyeka.


Lakini kitu cha aibu kimeila kazi ya baba zetu tokea ujana wetu; makundi yao ya kondoo na ng'ombe, wana wao na binti zao.


Na tulale kwa aibu yetu, haya yetu na itufunike; kwa maana tumemwasi BWANA, Mungu wetu, sisi na baba zetu, tangu ujana wetu hata leo; wala hatukuitii sauti ya BWANA, Mungu wetu.


Uangamivu baada ya uangamivu umetangazwa; kwa maana nchi yote imeharibika; hema zangu zimetekwa nyara ghafla, na mapazia yangu katika dakika moja.


Ee binti wa watu wangu, ujivike nguo ya magunia, na kugaagaa katika majivu; fanya maombolezo, kama maombolezo kwa ajili ya mwana wa pekee, maombolezo ya uchungu mwingi; maana mwenye kuteka nyara atakuja juu yetu ghafla.


Zikate nywele zako, Ee Yerusalemu, uzitupe, Ukafanye maombolezo juu ya vilele vya milima; Kwa maana BWANA amekikataa na kukitupa Kizazi cha ghadhabu yake.


Laiti kichwa changu kingekuwa maji, na macho yangu kuwa chemchemi ya machozi, ili nipate kulia mchana na usiku kwa ajili yao waliouawa wa binti ya watu wangu!


Kwa milima nitalia na kulalama, Na kwa malisho ya nyikani nitafanya maombolezo; Kwa sababu yameteketea, hata hakuna apitaye, Wala hapana awezaye kusikia sauti ya ng'ombe; Ndege wa angani, na wanyama wa mwituni, Wamekimbia, wamekwenda zao.


Lakini lisikieni neno la BWANA, enyi wanawake, Na masikio yenu yapokee neno la kinywa chake; Mkawafundishe binti zenu kuomboleza, Na kila mmoja jirani yake kulia.


Hulia sana wakati wa usiku, Na machozi yake yapo mashavuni; Miongoni mwa wote waliompenda Hakuna hata mmoja amfarijiye; Rafiki zake wote wamemtenda hila, Wamekuwa adui zake.


Macho yangu yamechoka kwa machozi, Mtima wangu umetaabika; Ini langu linamiminwa juu ya nchi Kwa uharibifu wa binti ya watu wangu; Kwa sababu watoto wachanga na wanyonyao, Huzimia katika mitaa ya mji.


Nikushuhudie nini? Nikufananishe na nini, Ee Binti Yerusalemu? Nikulinganishe na nini, nipate kukufariji, Ee bikira binti Sayuni? Kwa maana uvunjifu wako ni mkuu kama bahari, Ni nani awezaye kukuponya?


Mioyo yao ilimlilia Bwana; Ee ukuta wa binti Sayuni! Machozi na yachuruzike kama mto Mchana na usiku; Usijipatie kupumzika; Mboni ya jicho lako isikome.


Jicho langu lachuruzika mito ya machozi Kwa sababu ya kuharibiwa kwa binti zangu.


Kwa ajili ya hayo, asema BWANA, Mungu wa majeshi, aliye Bwana; Kutakuwako maombolezo katika njia kuu zote; nao watasema katika njia zote, Ole! Ole! Nao watamwita mkulima aje kuombolea, na hao walio hodari wa kulia waje kuomboleza.


Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo