Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 8:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

7 Naam, koikoi angani ajua nyakati zake zilizoamriwa; na hua na mbayuwayu na korongo huangalia wakati wa kuja kwao; bali watu wangu hawazijui amri za BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Hata korongo anajua wakati wa kuhama; njiwa, mbayuwayu na koikoi, hufuata majira yao ya kurudi. Lakini watu wangu hawa hawajui kitu juu ya amri zangu mimi Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Hata korongo anajua wakati wa kuhama; njiwa, mbayuwayu na koikoi, hufuata majira yao ya kurudi. Lakini watu wangu hawa hawajui kitu juu ya amri zangu mimi Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Hata korongo anajua wakati wa kuhama; njiwa, mbayuwayu na koikoi, hufuata majira yao ya kurudi. Lakini watu wangu hawa hawajui kitu juu ya amri zangu mimi Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Hata korongo aliye angani anayajua majira yake yaliyoamriwa, nao njiwa, mbayuwayu na koikoi hufuata majira yao ya kurudi. Lakini watu wangu hawajui Mwenyezi Mungu anachotaka kwao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Hata korongo aliyeko angani anayajua majira yake yaliyoamriwa, nao njiwa, mbayuwayu na koikoi hufuata majira yao ya kurudi. Lakini watu wangu hawajui bwana anachotaka kwao.

Tazama sura Nakili




Yeremia 8:7
10 Marejeleo ya Msalaba  

Maua yatokea katika nchi, Wakati wa kuimba umefika, Na sauti ya mwigo husikiwa kwetu.


Ng'ombe amjua bwana wake, Na punda ajua kibanda cha bwana wake; Bali Israeli hajui, watu wangu hawafikiri.


Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe.


Na kinubi, na zeze, na matari, na filimbi, na mvinyo, zote ziko katika karamu zao; lakini hawaiangalii kazi ya BWANA wala kuyafikiri matendo ya mikono yake.


Kwa maana watu wangu ni wapumbavu, hawanijui; ni watoto waliopungukiwa na akili, wala hawana ufahamu; ni wenye akili katika kutenda mabaya, bali katika kutenda mema hawana maarifa.


Basi, kwa hiyo, simba atokaye mwituni atawaua, mbwamwitu wa jioni atawateka, chui ataivizia miji yao, kila mtu atokaye humo atararuliwa vipande vipande; kwa sababu makosa yao ni mengi, na kurudi nyuma kwao kumezidi.


Kwa sababu hiyo sheria imelegea, wala hukumu haipatikani; kwa maana watu wabaya huwazunguka wenye haki; kwa sababu hiyo hukumu inayotolewa huwa imepotoshwa.


Ndipo nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, wanawake wawili walitokea, nao upepo ulikuwa katika mabawa yao; na mabawa yao yalikuwa kama mabawa ya korongo; wakaiinua ile efa kati ya dunia na mbingu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo