Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 8:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 Nilisikiliza nikasikia, lakini walisema yasiyo sawa; hapana mtu aliyetubia maovu yake, akisema, Nimefanya nini? Kila mtu hurudia mwendo wake mwenyewe, kama farasi aendavyo kasi vitani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Mimi nilisikiliza kwa makini, lakini wao hawakusema ukweli wowote. Hakuna mtu anayetubu uovu wake, wala kujiuliza; ‘Nimefanya nini?’ Kila mmoja wao anashika njia yake, kama farasi akimbiliavyo moja kwa moja vitani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Mimi nilisikiliza kwa makini, lakini wao hawakusema ukweli wowote. Hakuna mtu anayetubu uovu wake, wala kujiuliza; ‘Nimefanya nini?’ Kila mmoja wao anashika njia yake, kama farasi akimbiliavyo moja kwa moja vitani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Mimi nilisikiliza kwa makini, lakini wao hawakusema ukweli wowote. Hakuna mtu anayetubu uovu wake, wala kujiuliza; ‘Nimefanya nini?’ Kila mmoja wao anashika njia yake, kama farasi akimbiliavyo moja kwa moja vitani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Nimewasikiliza kwa makini, lakini hawataki kusema lililo sawa. Hakuna anayetubu makosa yake akisema, “Nimefanya nini?” Kila mmoja hufuata njia yake mwenyewe kama farasi anayeenda vitani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Nimewasikiliza kwa makini, lakini hawataki kusema lililo sawa. Hakuna anayetubia makosa yake akisema, “Nimefanya nini?” Kila mmoja hufuata njia yake mwenyewe kama farasi anayekwenda vitani.

Tazama sura Nakili




Yeremia 8:6
24 Marejeleo ya Msalaba  

Nitamwambia Mungu, Usinihukumie makosa; Nijulishe kwa nini unapingana nami.


Kwani kuna mtu aliyemwambia Mungu, Mimi nimevumilia kurudiwa, ingawa sikukosa;


Nisiyoyaona nifundishe wewe; Kama nimefanya uovu sitafanya tena?


Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye hekima, Amtafutaye Mungu.


Kwa ajili ya hayo BWANA atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana BWANA ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao.


Kwa sababu ya uovu wa kutamani kwake niliona hasira, nikampiga; nilificha uso wangu, nikaona ghadhabu; naye akaendelea kwa ukaidi, kuifuata njia ya moyo wake mwenyewe.


Akaona ya kuwa hapana mtu, akastaajabu kwa kuwa hapana mwombezi; basi, mkono wake mwenyewe ndio uliomletea wokovu; na haki yake ndiyo iliyomsaidia.


Nimesikia waliyoyasema manabii wanaotabiri uongo kwa jina langu, wakisema, Nimeota ndoto; nimeota ndoto.


Je! Ataishika hasira yake hata milele? Ataishika hata mwisho? Tazama, umesema hivyo, bali umetenda mambo mabaya, umefuata njia yako mwenyewe.


Pigeni mbio huku na huku katika njia za Yerusalemu, mkaone sasa, na kujua, na kutafuta katika viwanja vyake, kwamba mwaweza kumpata mtu mmoja, kwamba yuko mtu mmoja awaye yote atendaye kwa haki, atafutaye uaminifu; nami nitausamehe mji huo.


Kwa sababu atafakari, na kughairi, na kuyaacha makosa yake yote aliyoyatenda, hakika ataishi, hatakufa.


Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.


Naam, Israeli wote wameivunja sheria yako, kwa kugeuka upande, wasiisikilize sauti yako; basi kwa hiyo laana imemwagwa juu yetu, na kiapo kile kilioandikwa katika Sheria ya Musa, mtumishi wa Mungu; kwa sababu tumemtenda dhambi.


Mtu amchaye Mungu ametoweka, asionekane katika nchi, wala hapana mtu mwenye adili katika wanadamu; wote huotea ili kumwaga damu; kila mtu humwinda ndugu yake kwa wavu.


Nilisema, Hakika utaniogopa, utakubali kurudiwa; ili yasikatiliwe mbali makao yake, sawasawa ya yote niliyoagiza katika habari zake; lakini waliondoka mapema na kuyaharibu matendo yao yote.


Basi sasa, BWANA wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.


BWANA wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.


Ndipo wale waliomcha BWANA waliposemezana wao kwa wao. Naye BWANA akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha BWANA, na kulitafakari jina lake.


Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyodhani anakawia, bali huwavumilia, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba.


Na wanadamu waliobakia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wala kutembea.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo