Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 8:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Tena utawaambia, BWANA asema hivi, Je! Watu wataanguka, wasisimame tena? Je! Mtu atageuka aende zake, asirudi tena?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 “Wewe Yeremia utawaambia kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Mtu akianguka, je hainuki tena? Mtu akipotea, je, hairudii tena njia yake?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 “Wewe Yeremia utawaambia kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Mtu akianguka, je hainuki tena? Mtu akipotea, je, hairudii tena njia yake?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 “Wewe Yeremia utawaambia kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Mtu akianguka, je hainuki tena? Mtu akipotea, je, hairudii tena njia yake?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 “Waambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: “ ‘Je, watu wanapoanguka hawainuki? Je, mtu anapopotea harudi?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 “Waambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo bwana: “ ‘Je, watu wanapoanguka hawainuki? Je, mtu anapopotea harudi?

Tazama sura Nakili




Yeremia 8:4
15 Marejeleo ya Msalaba  

maombi yoyote au dua yoyote ikifanywa na mtu yeyote, au na watu wako Israeli wote pamoja, watakaojua kila mtu maradhi ya moyo wake, na kuikunjua mikono yake kuielekea nyumba hii;


Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya.


Nimeyafuta makosa yako kama wingu zito, na dhambi zako kama wingu; unirudie; maana nimekukomboa.


Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.


Katika manabii wa Yerusalemu nimeona neno linalochukiza sana; hufanya zinaa; huenda katika maneno ya uongo, hutia nguvu mikono ya watendao maovu, hata ikawa hapana mtu arejeaye na kuuacha uovu wake; wote pia wamekuwa kama Sodoma kwangu, na wenyeji wake kama Gomora.


Watu husema, Mtu akimwacha mkewe, naye akienda zake, akawa mke wa mtu mwingine, je! Mtu huyo atamrudia tena? Je! Nchi hiyo haitatiwa unajisi? Lakini wewe umefanya mambo ya ukahaba na wapenzi wengi; nawe, je! Utanirudia mimi? Asema BWANA.


Rudini, enyi watoto waasi, mimi nitaponya maasi yenu. Tazama, tumekuja kwako; maana wewe u BWANA, Mungu wetu.


Huenda nyumba ya Yuda watasikia mabaya yote niliyokusudia kuwatenda; wapate kurudi, kila mtu akaiache njia yake mbaya; nami nikawasamehe uovu wao na dhambi yao.


Kama ukitaka kurudi, Ee Israeli, asema BWANA, utanirudia mimi; na kama ukitaka kuyaondoa machukizo yako, yasiwe mbele ya macho yangu, ndipo hutaondolewa;


Je! Mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? Asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi?


Ee Israeli, mrudie BWANA, Mungu wako; maana umeanguka kwa sababu ya uovu wako.


Njooni, tumrudie BWANA; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga majeraha yetu.


Na kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; ila hata hivyo hawakumrudia BWANA, Mungu wao, wala hawakumtafuta kwa ajili ya hayo yote.


Bikira wa Israeli ameanguka; hatainuka tena; Ameangushwa katika nchi yake; hakuna mtu wa kumwinua.


Usifurahi juu yangu, Ee adui yangu; niangukapo, nitasimama tena; nikaapo gizani, BWANA atakuwa nuru kwangu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo