Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 8:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Tazama, sauti ya kilio cha binti ya watu wangu, itokayo katika nchi iliyo mbali sana; Je! BWANA hayumo katika Sayuni? Mfalme wake hayumo ndani yake? Mbona wamenikasirisha kwa sanamu zao walizochonga, na kwa ubatili wa kigeni?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Sikiliza kilio cha watu wangu, kutoka kila upande katika nchi. “Je, Mwenyezi-Mungu hayuko Siyoni? Je, mfalme wake hayuko tena huko?” “Mbona wamenikasirisha kwa sanamu zao za miungu, na vinyago vyao vya miungu ya kigeni?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Sikiliza kilio cha watu wangu, kutoka kila upande katika nchi. “Je, Mwenyezi-Mungu hayuko Siyoni? Je, mfalme wake hayuko tena huko?” “Mbona wamenikasirisha kwa sanamu zao za miungu, na vinyago vyao vya miungu ya kigeni?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Sikiliza kilio cha watu wangu, kutoka kila upande katika nchi. “Je, Mwenyezi-Mungu hayuko Siyoni? Je, mfalme wake hayuko tena huko?” “Mbona wamenikasirisha kwa sanamu zao za miungu, na vinyago vyao vya miungu ya kigeni?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Sikia kilio cha watu wangu kutoka nchi ya mbali: “Je, Mwenyezi Mungu hayuko Sayuni? Je, Mfalme wake hayuko tena huko?” “Kwa nini wamenikasirisha kwa vinyago vyao, kwa sanamu zao za kigeni zisizofaa?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Sikia kilio cha watu wangu kutoka nchi ya mbali: “Je, bwana hayuko Sayuni? Je, Mfalme wake hayuko tena huko?” “Kwa nini wamenikasirisha kwa vinyago vyao, kwa sanamu zao za kigeni zisizofaa?”

Tazama sura Nakili




Yeremia 8:19
35 Marejeleo ya Msalaba  

Na ahimidiwe BWANA toka Sayuni, Akaaye Yerusalemu. Haleluya.


Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, Tukalia tulipoikumbuka Sayuni.


BWANA atamiliki milele, Mungu wako, Ee Sayuni, kwa vizazi vyote. Haleluya.


Israeli na amfurahie Yeye aliyemwumba, Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao.


Nawachukia wao washikao yasiyofaa yenye uongo; Bali mimi namtumainia BWANA.


Ole wake, taifa lenye dhambi, watu wanaochukua mzigo wa uovu, wazao wa watenda mabaya, watoto wanaoharibu; wamemwacha BWANA, wamemdharau yeye aliye Mtakatifu wa Israeli, wamefarakana naye na kurudi nyuma.


Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni; Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.


watu waliotoka katika nchi iliyo mbali, tokea upande wa mwisho wa mbingu; naam, BWANA na silaha za ghadhabu yake, ili aiangamize nchi yote.


Kwa maana BWANA ndiye mwamuzi wetu; BWANA ndiye mfanya sheria wetu; BWANA ndiye mfalme wetu; ndiye atakayetuokoa.


Ndipo Isaya nabii akamwendea mfalme Hezekia, akamwambia, Watu hawa walisema nini? Nao wametoka wapi kuja kwako? Hezekia akasema, Wametoka katika nchi iliyo mbali, wakaja kwangu toka Babeli.


Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako Asiyetahiriwa, wala aliye najisi.


Ni ubatili tu, ni kazi za udanganyifu; Wakati wa kujiliwa kwao watapotea.


Je! Umemkataa Yuda kabisa? Roho yako imeichukia Sayuni? Mbona umetupiga, tusiwe na dawa ya kutuponya? Tulitazamia amani, lakini hayakuja mema yoyote, tulitazamia wakati wa kupona, na tazama, kufadhaika tu!


Kwa nini wewe umekuwa kama mtu aliyeshtuka, kama shujaa asiyeweza kuokoa? Lakini wewe, BWANA, u katikati yetu, nasi tunaitwa kwa jina lako; usituache.


BWANA asema hivi, Baba zenu waliona dhuluma gani kwangu, hata wakafarakana nami, wakafuata ubatili, nao wakawa ubatili?


maana wanawatabiria uongo, ili kuwatoa ninyi mbali na nchi yenu; niwafukuze mkaangamie.


Maana kutakuwa siku moja, ambayo walinzi watalia juu ya vilima vya Efraimu, Inukeni, tukaende Sayuni, kwa BWANA, Mungu wetu.


Maana wana wa Israeli, na wana wa Yuda, wametenda yaliyo mabaya tu mbele za uso wangu, tangu ujana wao; maana wana wa Israeli wamenichokoza tu kwa matendo ya mikono yao, asema BWANA.


Je! Watu hawa wanikasirisha mimi? Asema BWANA; hawajikasirishi nafsi zao, na kuzitia haya nyuso zao wenyewe?


Mavuno yamepita, wakati wa joto umekwisha, wala sisi hatukuokoka.


Nami nitawatawanya kati ya mataifa, ambao wao hawakuwajua; wala baba zao, nami nitatuma upanga nyuma yao, hata nitakapowaangamiza kabisa.


Kuuzunguka ni mianzi elfu kumi na nane; na jina la mji huo tangu siku hiyo litakuwa hili, BWANA yupo.


Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la BWANA ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama BWANA alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao BWANA.


Nami nitaitakasa damu yao ambayo sijaitakasa; kwa maana BWANA ndiye akaaye Sayuni.


Bali katika mlima Sayuni kutakuwa na watakaookoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki tena milki zao.


Sasa mbona unapiga kelele? Je! Hakuna mfalme kwako, mshauri wako amepotea, hata umeshikwa na uchungu kama mwanamke wakati wa kuzaa?


BWANA ameziondoa hukumu zako, Amemtupa nje adui yako; Mfalme wa Israeli, naam, yeye BWANA, yuko katikati yako; Hutaogopa uovu tena.


Kwa maana, tazama, nitatikisa mkono wangu juu yao, nao watakuwa mateka ya hao waliowatumikia; nanyi mtajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma.


wakisema, Akina bwana, mbona mnafanya haya? Sisi nasi tu wanadamu hali moja na ninyi; tunawahubiria Habari Njema, ili mgeuke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo;


Ndipo hasira yangu itakapowaka juu yao siku hiyo, nami nitawaacha, nitawaficha uso wangu, nao wataliwa, tena watajiliwa na mambo maovu mengi na mashaka; hata waseme siku hiyo, Je! Kujiliwa kwetu na maovu haya si kwa sababu Mungu wetu hayumo kati yetu?


Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kulia, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo