Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 8:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 Mbona tunakaa kimya? Jikusanyeni, tukaingie ndani ya miji yenye maboma, tukanyamaze humo kwa maana BWANA, Mungu wetu, ametunyamazisha, naye ametupa maji yenye uchungu tunywe, kwa sababu tumemwasi BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 “Watu wanauliza: Kwa nini sisi tunakaa tu hapa? Kusanyikeni, tuingie katika miji yenye ngome, tukaangamie huko! Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ametupangia tuangamie, ametupa maji yenye sumu tunywe, kwa kuwa tumemkosea yeye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 “Watu wanauliza: Kwa nini sisi tunakaa tu hapa? Kusanyikeni, tuingie katika miji yenye ngome, tukaangamie huko! Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ametupangia tuangamie, ametupa maji yenye sumu tunywe, kwa kuwa tumemkosea yeye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 “Watu wanauliza: Kwa nini sisi tunakaa tu hapa? Kusanyikeni, tuingie katika miji yenye ngome, tukaangamie huko! Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ametupangia tuangamie, ametupa maji yenye sumu tunywe, kwa kuwa tumemkosea yeye.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Kwa nini tunaketi hapa? Kusanyikeni pamoja! Tukimbilie kwenye miji yenye ngome, tukaangamie huko! Kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, ametuhukumu kuangamia, na kutupatia maji yenye sumu tunywe, kwa sababu tumemtenda dhambi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 “Kwa nini tunaketi hapa? Kusanyikeni pamoja! Tukimbilie kwenye miji yenye maboma, tukaangamie huko! Kwa kuwa bwana, Mungu wetu ametuhukumu kuangamia, na kutupa maji yenye sumu tunywe, kwa sababu tumemtenda dhambi.

Tazama sura Nakili




Yeremia 8:14
23 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Daudi akamwambia Abishai, Sasa Sheba, mwana wa Bikri, atatudhuru, kuliko Absalomu; twaa wewe watumishi wa bwana wako, ukamfuatie, asiingie katika miji yenye boma, na kutuponyoka.


Nilikuwa sisemi, nilinyamaa kimya, Sina faraja, maumivu yangu yakazidi.


Wakanipa uchungu kuwa chakula changu; Na nilipokuwa na kiu wakaninywesha siki.


Kaa kimya, ingia gizani, Ee binti wa Wakaldayo; Maana hutaitwa tena Malkia wa falme.


Ee BWANA, tunakiri uovu wetu, na ubaya wa baba zetu; maana tumekutenda dhambi.


Ijapokuwa maovu yetu yanatushuhudia, lakini utende wewe kwa ajili ya jina lako, Ee BWANA, maana kurudi nyuma kwetu ni kwingi; tumekutenda dhambi.


Basi BWANA wa majeshi asema hivi, kuhusu habari ya manabii, Tazama, nitawalisha pakanga, nitawanywesha maji ya uchungu; kwa kuwa kutoka kwa manabii hao wa Yerusalemu kukufuru kumeingia katika nchi yote.


Na tulale kwa aibu yetu, haya yetu na itufunike; kwa maana tumemwasi BWANA, Mungu wetu, sisi na baba zetu, tangu ujana wetu hata leo; wala hatukuitii sauti ya BWANA, Mungu wetu.


Lakini ikawa, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, alipopanda akaingia nchi hii, ndipo tukasema, Haya! Twende Yerusalemu, kwa kuliogopa jeshi la Wakaldayo, na kwa kuliogopa jeshi la Washami; ndiyo maana sasa tunaishi Yerusalemu.


bali wameenda katika ushupavu wa mioyo yao wenyewe, na kuandamana na Mabaali, kama walivyofundishwa na baba zao.


Basi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitawalisha pakanga, naam, watu hawa, nami nitawapa maji yenye sumu wayanywe.


Kumbuka mateso yangu, na msiba wangu, Pakanga na nyongo.


Ndipo Musa akamwambia Haruni, Jambo hili ni hilo BWANA alilolinena, akisema, Nitatakaswa mimi katika hao wanikaribiao, nami nitatukuzwa mbele ya watu hao wote. Haruni akanyamaza kimya.


Na mjomba wa mtu atakapomwinua, yaani, yeye amchomaye moto, ili atoe mifupa yake nyumbani, naye atakapomwambia yeye aliye katika pande za ndani za nyumba, Je! Yuko mtu yeyote pamoja nawe? Naye atakaposema, La, hapana; ndipo atasema, Nyamaza kimya; maana hatuna ruhusa kulitaja jina la BWANA.


Lakini BWANA yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake.


Nyamazeni, ninyi nyote wenye mwili, mbele za BWANA; kwa maana ameamka, na kutoka katika maskani yake takatifu.


wakampa kunywa divai iliyochanganyika na nyongo; lakini yeye alipoionja hakutaka kunywa.


asiwe mtu katikati yenu, mume wala mke, wala jamaa, wala kabila, ageukaye moyo wake leo amwache BWANA, Mungu wetu, kwenda kuitumikia miungu ya mataifa hayo; lisiwe katikati yenu shina lizaalo uchungu na pakanga;


Maana, mzabibu wao ni mzabibu wa Sodoma, Nao ni wa mashamba ya Gomora; Zabibu zao ni zabibu za uchungu, Vichala vyao ni vichungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo