Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 8:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Nitawaangamiza kabisa, asema BWANA; hapana zabibu katika mizabibu, wala tini katika mitini, hata jani lake litanyauka; na vitu vile nilivyowapa vitawapotea.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 “Mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Nilipotaka kukusanya chochote kutoka kwao, sikupata zabibu hata moja juu ya mzabibu, sikupata tini zozote juu ya mtini; hata majani yao yamekauka. Hata nilichokuwa nimewapa kimetoweka.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 “Mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Nilipotaka kukusanya chochote kutoka kwao, sikupata zabibu hata moja juu ya mzabibu, sikupata tini zozote juu ya mtini; hata majani yao yamekauka. Hata nilichokuwa nimewapa kimetoweka.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 “Mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Nilipotaka kukusanya chochote kutoka kwao, sikupata zabibu hata moja juu ya mzabibu, sikupata tini zozote juu ya mtini; hata majani yao yamekauka. Hata nilichokuwa nimewapa kimetoweka.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 “ ‘Nitayaondoa mavuno yao, asema Mwenyezi Mungu. Hapatakuwa zabibu kwenye mzabibu. Hapatakuwa na tini kwenye mtini, na majani yake yatanyauka. Kile nilichowapa watanyang’anywa.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 “ ‘Nitayaondoa mavuno yao, asema bwana. Hapatakuwepo zabibu kwenye mzabibu. Hapatakuwepo na tini kwenye mtini, majani yake yatanyauka. Kile nilichowapa watanyang’anywa.’ ”

Tazama sura Nakili




Yeremia 8:13
25 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana shamba la mizabibu la eka kumi litatoa bathi moja tu, na homeri ya mbegu itatoa efa tu.


Wafungapo, mimi sitasikia kilio chao; na watoapo sadaka za kuteketezwa na sadaka ya unga, sitazitakabali; bali nitawaangamiza kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni.


Basi, kwa hiyo BWANA asema hivi, Kwa habari za manabii wanaotabiri kwa jina langu, wala mimi sikuwatuma, lakini husema, Upanga na njaa havitaingia katika nchi hii; Kwa upanga na njaa manabii hao wataangamizwa.


Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa joto ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.


Nao watakula mavuno yako, na mkate wako, ambao iliwapasa wana wako na binti zako kuula; watakula makundi yako ya kondoo na ya ng'ombe; watakula mizabibu yako na mitini yako; wataiharibu miji yako yenye boma, uliyokuwa ukiitumainia, naam, wataiharibu kwa upanga.


Kwa hiyo, Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, hasira yangu na ghadhabu yangu zitamwagwa juu ya mahali hapa, juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya miti ya mashamba, na juu ya mazao ya nchi; nayo itateketea, isizimike.


Kwa sababu hiyo nimemwaga ghadhabu yangu juu yao; nimewateketeza kwa moto wa hasira yangu; nami nimeileta njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao, asema Bwana MUNGU.


Nami nitaiharibu mizabibu yake na mitini yake, ambayo alisema, Hii ndiyo ujira wangu niliopewa na wapenzi wangu; nami nitaifanya kuwa msitu, na wanyama wa mashamba wataila.


Ameuharibu mzabibu wangu; ameuvunja mtini wangu; ameyaambua magamba yake kabisa; ameuangusha chini; matawi yake yamefanywa kuwa meupe.


na nguvu zenu mtazitumia bure; kwa kuwa nchi yenu haitazaa mazao yake, wala miti ya nchi haitazaa matunda yake.


Maana mtini hautachanua maua, Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; Taabu ya mzeituni itakuwa bure, Na mashamba hayatatoa chakula; Zizini hamtakuwa na kundi, Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng'ombe;


Nami nikaita wakati wa joto uje juu ya nchi, na juu ya milima, na juu ya nafaka, na juu ya divai mpya, na juu ya mafuta, na juu ya kila kitu itoacho nchi, na juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya kazi zote za mikono.


Niliwapiga kwa ukavu, na ukungu, na mvua ya mawe, katika kazi zote za mikono yenu; lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA.


Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi.


Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara.


Maana jua huchomoza kwa joto kali, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo