Yeremia 7:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC13 Na sasa, kwa sababu mmezifanya kazi hizi zote asema BWANA, nami nikasema nanyi, nikiamka mapema na kunena, lakini hamkusikia; nami nikawaita wala hamkuniitikia; Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema13 Nyinyi mmefanya mambo hayo yote, na hata niliposema nanyi tena na tena hamkunisikiliza. Nilipowaiteni hamkuitika. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND13 Nyinyi mmefanya mambo hayo yote, na hata niliposema nanyi tena na tena hamkunisikiliza. Nilipowaiteni hamkuitika. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza13 Nyinyi mmefanya mambo hayo yote, na hata niliposema nanyi tena na tena hamkunisikiliza. Nilipowaiteni hamkuitika. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu13 Mlipokuwa mnafanya haya yote, asema Mwenyezi Mungu, nilisema nanyi tena na tena, lakini hamkusikiliza; niliwaita, lakini hamkujibu. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu13 Mlipokuwa mnafanya yote haya, asema bwana, nilisema nanyi tena na tena, lakini hamkusikiliza; niliwaita, lakini hamkujibu. Tazama sura |
Basi, nilipokuja, mbona hapakuwa na mtu? Nilipoita, mbona hapakuwa na mtu aliyenijibu? Je! Mkono wangu ni mfupi, hata nisiweze kukomboa? Au je! Mimi sina nguvu za kuponya? Tazama, kwa kukemea kwangu naikausha bahari, mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wanuka kwa sababu hapana maji, nao wafa kwa kiu.
Pia niliwatuma watumishi wangu wote, manabii, kwenu ninyi, nikiwatuma pasipo kukoma, nikisema, Rudini sasa, kila mtu na aiache njia yake mbaya, mkatengeneze matendo yenu, wala msiifuate miungu mingine, ili kuitumikia, nanyi mtakaa katika nchi hii, niliyowapa ninyi na baba zenu; lakini hamkutega masikio yenu, wala hamkunisikiliza.