Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 7:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Lakini nendeni sasa hadi mahali pangu palipokuwapo katika Shilo, nilipolikalisha jina langu hapo kwanza, mkaone nilivyopatenda kwa sababu ya uovu wa watu wangu Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Nendeni mahali pangu kule Shilo, mahali nilipopachagua niabudiwe hapo awali, mkaone maangamizi niliyoyafanya huko kwa sababu ya uovu wa watu wangu, Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Nendeni mahali pangu kule Shilo, mahali nilipopachagua niabudiwe hapo awali, mkaone maangamizi niliyoyafanya huko kwa sababu ya uovu wa watu wangu, Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Nendeni mahali pangu kule Shilo, mahali nilipopachagua niabudiwe hapo awali, mkaone maangamizi niliyoyafanya huko kwa sababu ya uovu wa watu wangu, Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 “ ‘Nendeni sasa mahali pangu palipokuwa huko Shilo, ambapo nilipafanya pa kwanza kuwa makao ya Jina langu, nanyi mwone lile nililopafanyia kwa ajili ya uovu wa watu wangu Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 “ ‘Nendeni sasa mahali pangu palipokuwa huko Shilo, mahali ambapo nilipafanya pa kwanza kuwa makao ya Jina langu, nanyi mwone lile nililopafanyia kwa ajili ya uovu wa watu wangu Israeli.

Tazama sura Nakili




Yeremia 7:12
13 Marejeleo ya Msalaba  

basi nitawakatilia Israeli mbali na nchi hii niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli watakuwa mithali na neno la tusi katika mataifa yote.


basi, nitafanya nyumba hii kuwa kama Shilo, na mji huu nitaufanya kuwa laana kwa mataifa yote ya dunia.


basi, nitaitenda nyumba hii, iitwayo kwa jina langu, mnayoitumainia, na mahali hapa nilipowapa ninyi na baba zenu, kama nilivyopatenda Shilo.


wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa BWANA.


Lakini mahali atakapochagua BWANA, Mungu wenu, katika makabila yenu yote, apaweke jina lake, maana, ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo, nawe uende huko;


Kisha mkutano mzima wa wana wa Israeli walikutana pamoja hapo Shilo, wakasimamisha hema ya kukutania huko; nayo nchi ilikuwa imeshindwa mbele zao.


Kisha Yoshua akapiga kura kwa ajili yao hapo mbele za BWANA katika Shilo; huko Yoshua akawagawanyia wana wa Israeli hiyo nchi sawasawa na mafungu yao.


Basi wakaiabudu hiyo sanamu ya kuchonga aliyotengeneza Mika, wakati wote ile nyumba ya Mungu ilipokuwako huko Shilo.


Na mtu huyo alikuwa akikwea kutoka mjini kwake mwaka kwa mwaka, ili kuabudu, na kumtolea BWANA wa majeshi dhabihu katika Shilo. Na wale wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, makuhani wa BWANA, walikuwako huko.


Naam, akasema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; maana sanduku la Mungu limetwaliwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo