Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 6:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 Maana BWANA wa majeshi asema hivi, Jikatieni miti, mjenge boma juu ya Yerusalemu. Mji huu ni mji unaojiwa; dhuluma tupu imo ndani yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema: “Kateni miti yake, rundikeni udongo kuuzingira Yerusalemu. Mji huu ni lazima uadhibiwe, maana hamna lolote ndani yake ila dhuluma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema: “Kateni miti yake, rundikeni udongo kuuzingira Yerusalemu. Mji huu ni lazima uadhibiwe, maana hamna lolote ndani yake ila dhuluma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema: “Kateni miti yake, rundikeni udongo kuuzingira Yerusalemu. Mji huu ni lazima uadhibiwe, maana hamna lolote ndani yake ila dhuluma.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Kateni miti mjenge boma kuzingira Yerusalemu. Mji huu ni lazima uadhibiwe; umejazwa na uonevu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Hivi ndivyo asemavyo bwana Mwenye Nguvu Zote: “Kateni miti mjenge boma kuzunguka Yerusalemu. Mji huu ni lazima uadhibiwe, umejazwa na uonevu.

Tazama sura Nakili




Yeremia 6:6
15 Marejeleo ya Msalaba  

Basi, BWANA asema hivi kuhusu mfalme wa Ashuru, Yeye hataingia ndani ya mji huu, wala hatapiga mshale hapa, wala hatakuja mbele yake kwa ngao, wala hatajenga boma juu yake.


Maana kila ninenapo napiga kelele, nalia, Dhuluma na uharibifu! Kwa kuwa neno la BWANA limefanywa shutumu kwangu, na dhihaka, mchana kutwa.


Bali macho yako na moyo wako hauna utakalo ila kutamani, na kumwaga damu isiyo na hatia, na kudhulumu, na kutenda jeuri.


angalia maboma haya; wameujia mji huu ili kuutwaa; na mji huu umetiwa katika mikono ya Wakaldayo wanaopigana nao, kwa sababu ya upanga, na njaa, na tauni; na hayo uliyosema yamekuwa; na, tazama, wewe unayaona.


Kwa kuwa mji huu umekuwa sababu ya kunitia hasira, na sababu ya ghadhabu yangu, tangu siku ile walipoujenga hata siku hii ya leo; ili niuondoe usiwe mbele za uso wangu;


Maana BWANA, Mungu wa Israeli asema hivi, kuhusu nyumba za mji huu, na kuhusu nyumba za wafalme wa Yuda, zilizobomolewa ili kuyapinga maboma na upanga;


Hata ikawa, Yerusalemu ulipotwaliwa, (katika mwaka wa tisa wa Sedekia, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, na jeshi lake lote, wakaja juu ya Yerusalemu, wakauzingira;


Je! Nisiwapatilize kwa mambo hayo? Asema BWANA; na nafsi yangu, je! Nisijilipizie kisasi juu ya taifa la namna hii?


Je! Nisiwapatilize kwa sababu ya mambo hayo? Asema BWANA; na nafsi yangu, je! Nisijilipizie kisasi juu ya taifa la namna hii?


ukauhusuru, ukajenge ngome juu yake, na kufanya boma juu yake; ukaweke makambi juu yake, na kuweka magogo ya kuubomoa yauzunguke pande zote.


Bwana MUNGU asema hivi; Huu ndio Yerusalemu; nimeuweka kati ya mataifa, na nchi zauzunguka pande zote.


Basi mfalme wa kaskazini atakuja, na kufanya kilima, na kuupiga mji wenye maboma; na silaha za kusini hazitaweza kumpinga, wala watu wake wateule, wala hapatakuwa na nguvu za kumpinga.


Ole wake yeye aliyeasi na kutiwa unajisi, mji wa udhalimu!


Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo