Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 6:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 Basi, kwa hiyo, BWANA asema hivi, Tazama, nitaweka makwazo mbele ya watu hawa, na baba na wana wao watajikwaa pamoja; jirani ya mtu na rafiki yake watapotea.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Kwa hiyo mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Tazama, nitawawekea watu hawa vikwazo ambavyo vitawakwaza na kuwaangusha chini. Akina baba na watoto wao wa kiume wataangamia, kadhalika na majirani na marafiki.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Kwa hiyo mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Tazama, nitawawekea watu hawa vikwazo ambavyo vitawakwaza na kuwaangusha chini. Akina baba na watoto wao wa kiume wataangamia, kadhalika na majirani na marafiki.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Kwa hiyo mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Tazama, nitawawekea watu hawa vikwazo ambavyo vitawakwaza na kuwaangusha chini. Akina baba na watoto wao wa kiume wataangamia, kadhalika na majirani na marafiki.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Kwa hiyo hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: “Nitaweka vikwazo mbele ya watu hawa. Baba na wana wao watajikwaa juu yake, majirani na rafiki wataangamia.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Kwa hiyo hivi ndivyo asemavyo bwana: “Nitaweka vikwazo mbele ya watu hawa. Baba na wana wao watajikwaa juu yake, majirani na marafiki wataangamia.”

Tazama sura Nakili




Yeremia 6:21
23 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa hiyo akaleta juu yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao kwa upanga nyumbani mwa patakatifu pao, asiwahurumie kijana wala mwanamwali, mzee wala mnyonge; akawatia wote mkononi mwake.


Naye atakuwa ni mahali patakatifu; bali ni jiwe la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa kwa nyumba za Israeli zote mbili, na mtego na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu.


Na wengi watajikwaa juu yake, na kuanguka na kuvunjika, na kunaswa na kukamatwa.


Nitawagonganisha, mtu na mwenzake, naam, baba za watu na watoto wao pamoja, asema BWANA; sitahurumia, wala sitaachilia, wala sitarehemu, hata nisiwaangamize.


Mtukuzeni BWANA, Mungu wenu, kabla hajaleta giza, na kabla miguu yenu haijakwaa juu ya milima yenye giza; na wakati mnapoitazamia nuru, kabla hajaigeuza kuwa kivuli cha mauti, na giza nene.


Kwa sababu hiyo, uwatoe watoto wao waone njaa, uwatoe nguvu za upanga ziwapate; wake zao wafiwe na watoto wao, na kufiwa na waume zao; wanaume wao wauawe, na vijana wao wapigwe kwa upanga vitani.


Lakini wewe, BWANA, unajua mashauri yao yote juu yangu, ya kuniua; usiwasamehe uovu wao, wala usifute dhambi yao mbele za macho yako; bali wakwazwe mbele zako; uwatende mambo wakati wa hasira yako.


Na baada ya hayo, asema BWANA, nitamtia Sedekia, mfalme wa Yuda, na watumishi wake, na watu wote waliosalia ndani ya mji huu, baada ya tauni ile, na upanga, na njaa, katika mkono wa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, na katika mikono ya adui zao, na katika mikono ya watu wale wanaowatafuta roho zao; naye atawaua kwa ukali wa upanga; hatawaachilia, wala hatawahurumia, wala hatawarehemu.


Je! Waliona aibu, walipokuwa wametenda machukizo? La! Hawakuona aibu kabisa, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi wataanguka miongoni mwao waangukao; wakati wa kujiliwa kwao wataangushwa chini, asema BWANA.


Tena mtu mwenye haki aiachapo haki yake, na kutenda uovu, nami nikaweka kikwazo mbele yake, atakufa; kwa sababu hukumwonya, atakufa katika uovu, wala matendo yake ya haki aliyoyatenda hayatakumbukwa; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.


Kwa sababu hiyo baba za watu watawala wana wao kati yako, nao wana watawala baba zao; nami nitafanya hukumu ndani yako, na hao wote waliosalia kwako nitawatawanya kwa pepo zote.


Nao wataangukiana wenyewe kwa wenyewe, kama mbele ya upanga, hapo ambapo hapana afukuzaye; wala hamtakuwa na nguvu za kusimama mbele ya adui zenu.


Na Daudi asema, Meza yao na iwe tanzi na mtego, Na kitu cha kuwakwaza, na malipo kwao;


kama ilivyoandikwa, Tazama, naweka katika Sayuni jiwe likwazalo, na mwamba uangushao; Na kila amwaminiye hatatahayarika.


Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha. Kwa maana hujikwaza kwa neno lile, wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo