Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 6:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Lakini nimejaa ghadhabu ya BWANA; nimechoka kwa kujizuia; imwageni juu ya watoto walio njiani, na juu ya kusanyiko la vijana pia; maana hata mume atatwaliwa pamoja na mkewe, mzee pamoja na yeye aliyetimiza siku zake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Nimejaa hasira ya Mwenyezi-Mungu dhidi yao. Nashindwa kuizuia ndani yangu. Mwenyezi-Mungu akaniambia: “Imwage hasira barabarani juu ya watoto na pia juu ya makundi ya vijana; wote, mume na mke watachukuliwa, kadhalika na wazee na wakongwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Nimejaa hasira ya Mwenyezi-Mungu dhidi yao. Nashindwa kuizuia ndani yangu. Mwenyezi-Mungu akaniambia: “Imwage hasira barabarani juu ya watoto na pia juu ya makundi ya vijana; wote, mume na mke watachukuliwa, kadhalika na wazee na wakongwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Nimejaa hasira ya Mwenyezi-Mungu dhidi yao. Nashindwa kuizuia ndani yangu. Mwenyezi-Mungu akaniambia: “Imwage hasira barabarani juu ya watoto na pia juu ya makundi ya vijana; wote, mume na mke watachukuliwa, kadhalika na wazee na wakongwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Lakini nimejaa ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, nami siwezi kuizuia. “Wamwagie watoto walio barabarani, na juu ya vijana wa kiume waliokusanyika; mume na mke watakumbwa pamoja ndani yake, hata nao wazee waliolemewa na miaka.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Lakini nimejaa ghadhabu ya bwana, nami siwezi kuizuia. “Wamwagie watoto walioko barabarani, na juu ya vijana waume waliokusanyika; mume na mke watakumbwa pamoja ndani yake, hata nao wazee waliolemewa na miaka.

Tazama sura Nakili




Yeremia 6:11
22 Marejeleo ya Msalaba  

Hata vijana watazimia na kuchoka, na vijana wanaume wataanguka;


Sikuketi katika mkutano wao wanaojifurahisha, wala sikufurahi, niliketi peke yangu kwa sababu ya mkono wako; kwa maana umenijaza ghadhabu.


Umenikataa mimi, asema BWANA, umerudi nyuma; ndiyo maana nimenyosha mkono wangu juu yako, na kukuangamiza; nimechoka kwa kughairi.


Kwa sababu hiyo, uwatoe watoto wao waone njaa, uwatoe nguvu za upanga ziwapate; wake zao wafiwe na watoto wao, na kufiwa na waume zao; wanaume wao wauawe, na vijana wao wapigwe kwa upanga vitani.


Nami nikisema, Sitamtaja, wala sitasema tena kwa jina lake; basi, ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia.


Je! Nisiwapatilize kwa sababu ya mambo hayo? Asema BWANA; na nafsi yangu, je! Nisijilipizie kisasi juu ya taifa la namna hii?


Kwa hiyo, Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, hasira yangu na ghadhabu yangu zitamwagwa juu ya mahali hapa, juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya miti ya mashamba, na juu ya mazao ya nchi; nayo itateketea, isizimike.


Lakini lisikieni neno la BWANA, enyi wanawake, Na masikio yenu yapokee neno la kinywa chake; Mkawafundishe binti zenu kuomboleza, Na kila mmoja jirani yake kulia.


Kwa maana mauti imepandia madirishani mwetu, imeingia majumbani mwetu; Ipate kuwakatilia mbali watoto walio nje, na vijana katika njia kuu.


Bwana amenitia mikononi mwao, Ambao siwezi kupingamana nao. Bwana amewafanya mashujaa wangu wote Kuwa si kitu kati yangu; Ameita mkutano mkuu kinyume changu Ili kuwaponda vijana wangu; Bwana amemkanyaga kama shinikizoni Huyo bikira binti Yuda.


Kijana na mzee hulala chini Katika njia kuu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wameanguka kwa upanga; Umewaua katika siku ya hasira yako; Umeua, wala hukuona huruma.


Uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Angalieni, nitapatia unajisi patakatifu pangu, fahari ya uwezo wenu, mahali pa kutamaniwa na macho yenu, ambapo roho zenu zinapahurumia na wana wenu na binti zenu, mliowaacha nyuma, wataanguka kwa upanga.


Basi roho ikaniinua, ikanichukua mahali pengine; nami nikaenda kwa uchungu, na hasira kali rohoni mwangu, na mkono wa BWANA ulikuwa juu yangu kwa nguvu.


Akaniambia, Mwanadamu, lisha tumbo lako, ulijaze tumbo lako kwa hili gombo nikupalo. Ndipo nikalila, nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu, kama utamu wa asali.


Waueni kabisa, wazee, na viijana, na wasichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu yeyote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.


Bali mimi, hakika nimejaa nguvu kwa Roho ya BWANA; nimejaa hukumu na uwezo; nimhubirie Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake.


Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.


Paulo alipokuwa akiwangojea huko Athene na kuona jinsi mji ule ulivyojaa sanamu, roho yake ilichukizwa sana ndani yake.


Hata Sila na Timotheo walipoteremka kutoka Makedonia, Paulo akasongwa sana na lile neno, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo.


maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.


Nikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Nendeni mkayamwage yale mabakuli saba ya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo